SUAMEDIA

Ulemavu si kigezo cha kumfanya Mwanafunzi kushindwa kusonga mbele- Prof. Muhairwa

 

 Na: Tatyana Celestine, Winfrida Nicolaus

Imeelezwa kuwa Ulemavu si kigezo cha kumfanya Mwanafunzi kushindwa kusonga mbele kielimu na kuyafikia malengo yake kwani jamii inayomzunguka  inatakiwa kumjali na kumuongoza katika hatua stahiki kama wanafunzi wengine.   



Kauli hiyo imetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Utawala na Fedha SUA Prof. Amandus Muhairwa wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wanataaluma wa Chuo hicho juu ya kutambua na kujua namna ya kumuhudumia mtu mwenye mahitaji maalum ili kuleta usawa kwenye nyanja ya ufundishaji na ujifunzaji.

Prof. Muhairwa amesema hapo zamani SUA haikuchukua wanafunzi wenye mahitaji maalum lakini sasa enzi hizo zimekwisha pita hivyo mafunzo hayo yamepanda mbegu ya kutosha kuweza  kukiwezesha chuo kwenda mbele katika kutoa elimu jumuishi bila kujali hali ambazo wanafunzi hao wanakuwa nazo na malengo yao kuweza kutumia.

                         

Aidha amesema katika Mradi wa HEET mahitaji maalumu ni moja ya kipaumbele katika kuweka miundo mbinu ambayo wanaijenga na mingine iliyopo itaboreshwa kwa uwezo wa kuchukua watu wenye mahitaji maalum Pamoja na kuhakikisha watu hao wanaweza kujifunza bila tatizo lolote.

“Najua kama wakufunzi mmefundishwa mbinu za kufundisha watu wenye mahitaji maalum lakini pis jinsi ya kuwatahini  watu hao na semina kama hii Mradi wa HEET imeupatia uzito mkubwa sana  maka kuhakikisha mambo haya yanafika mpaka kwenye Mitaala ili kuhakikisha mazingira ya kujifunzia yanakuwa salama na rafiki kwa watu wa aina zote. ”, amesema Prof. Muhairwa

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Shule Kuu ya Elimu Idara ya Saikolijia na Mafunzo ya Mitaala Dkt. Lwimiko Sanga amesema mtu mwenye mahitaji maalum akipewa nafasi ya kufundishwa na kuelekezwa anaweza kufanya zaidi ya matarajio ja jamii kwakuwa wao pia wanauwezo wa kuajiliwa, ubunifu na hata kufanya vitu vya aina mbalimbali endapo watapewa nafasi na kuwezeshwa.

                                      

Aidha amesema wanafunzi wenye mahitaji maalum kipindi cha nyuma wamekuwa wakiacha  nyuma hasa katika masuala ya elimu kwa kuamini kuwa watu hao hawana uwezo wa kufanya lolote lakini ukweli ni kwama wana uwezo wa kufanya vitu mbali mbali kama walivyo wanafunzi wengine kama watapatiwa mazingira na nyenzo sahihi katika kupata elimu yao.

“Kimsingi walimu au wakufunzi wanaelekezwa namna ambavyo wanaweza kuyatambua haya mahitaji kwasababu wanafunzi wenye mahitaji maalum ni wengi na mahitaji yenyewe ni mengi na kila mahitaji yana namna yake maalum ya kuweza kuyatambua na kuwahudumia hivyo wanataaluma wanapitishwa eneo moja baada ya lingine ili kuweza kujua namna ya kutoa huduma stahiki na huyu mwanafunzi kuweza kunufaika na mafunzo anayoyapata”, amesema Dkt. Sanga

Naye mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Bw. Anthony Muhando kutoka Idara ya Upasuaji na Uzalishaji Wanyama  iliyopo  Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi Shirikishi  SUA amesema mafunzo hayo ni msaada mkubwa  kwa wakufunzi ambao wanakutana na wanafunzi mara kwa mara hivyo yatawasaidia kuwatambua watu wenye mahitaji maalum chuoni na kuboresha namna ya ufundishaji wao kwa lengo la kuleta usawa.

                          














Post a Comment

0 Comments