Na: Siwema Malibiche
Wafanyakazi katika vitengo vya
uzalishaji Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), wametakiwa kuzingatia mafunzo waliyopata
ili kukuza ubora wa huduma na bidhaa zinazotolewa SUA.
Rasi wa ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara kutoka SUA Dkt. Damas Philip akifunga mafunzo ya vitengo vya uzalishaji SUA (Picha zote na Ayoub Mwigune) |
Hayo yamesemwa na Rasi wa ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara kutoka SUA
Dkt. Damas Philip alipokuwa akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo kutoka vitengo zaidi ya 45 vya uzalishaji walioshiki mafunzo ya siku mbili katika Kampasi ya Edward Moringe mkoani Morogoro .
Amesema SUA ni miongoni mwa Taasisi
za Serikali zenye rasilimali nyingi
ambazo zinatakiwa kutumiwa kwa usahihi
ili kuleta tija chuoni na taifa kwa
ujumla kwa kuongeza uzalishaji katika
vitengo vilivyopo ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji.
“Nimefurahi kusikia kuwa wawezeshaji ambao wametumika katika mafunzo haya
wametoka ndani ya chuo ambao wanakifahamu chuo vizuri na fursa zilizopo na hii imeonyesha namna nzuri
ya kutumia rasilimali tulizonazo kwa kuleta maendeleeo kwa taasisi na nina
amini mafunzo haya ya siku mbili hayajapotea
bure na kila kitu kitatiliwa maanani ”,
amesema Dkt. Philip.
Naye, Suma Mwakanenela kutoka Ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara ambae alikuwa muwezeshaji wa mafunzo hayo,
amesema kuwa mafunzo hayo yatasaida kukuza uzalishaji katika vitengo mbalimbali
ndani ya SUA, iwapo yatafanyiwa kazi kwa kuongeza ubora kwa kutumia ubunifu na fursa ipasavyo ili kuongeza uzalishaji.
Suma Mwakanenela kutoka Ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara ambae alikuwa muwezeshaji akifafanua namna mafunzo hayo yatakavyosaidia katika uzalishaji SUA |
Kwa upande wake mmoja wa washiriki katika mafunzo hayo Bakari Mohamed Abdallah kutoka Shule Kuu ya Uhandisi na Teknolojia SOET amewashukuru, waandaaji wa mafunzo hayo kwa
kuwaongezea uelewa wa namna nzuri ya kutumia fursa na amekiri kujua vitu vingi ambavyo awali
hakuwa akivijua mfano matumuizi ya busara katika utoaji huduma kwa wateja.
Naye Grace Kajuna Afisa Utumishi kutoka Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza, ICE SUA amesema mafunzo hayo yamemuongezea uelewa hasa namna mzuri ya kutumia fursa zilizopo
kwenye kuongeza pato la Chuo na
anatatarajia kuboresha huduma anazozifanya katika kitengo chake na ameahidi kuyatekeleza
yote aliyojifunza katika uzalishaji.
Picha chini ni wafanyakazi katika vitengo vya uzalishaji SUA 👇
0 Comments