Na: Tatyana Celestine, Winfrida Nicolaus
Imeelezwa kuwa ni vyema kutengeneza Mitaala yenye kuzingatia uwezo ili kumuwezesha muhitimu wa Chuo Kikuu kuhitimu akiwa tayari kwenda kufanya kazi kulingana na vigezo vya mahitaji ya soko la ajira na sio kuwa na shaada pekee.
Amebainisha
hayo Mtaalam wa Mitaala kutoka nchini Uganda Dkt. Gillian Kasirye wakati
akizungumza na SUAMEDIA kwenye Mafunzo yaliyowakutanisha Wataalamu kutoka Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo pamoja na wajumbe kutoka Mtandao wa Vyuo Vikuu vya Kilimo katika nchi
za Afrika (RUFORUM) ambapo amesema walimu wengi wanalijua somo lakini hawajui jinsi
ya kubuni kwa namna ambayo litawashawishi
wanafunzi kuelewa.
Amesema kila chuo kina kitivo na kozi tofauti ni kawaida kubeba taarifa nyingi ikiwemo za kinadharia, lakini pia maudhui mengi hivyo wanapoongelea kuhusu uwezo kujumuishwa katika Mafunzo ikiwemo kuzingatiwa kwa wanafunzi, kufundishwa kupokea ujuzi, maarifa na mitazamo ili wanapohitimu wakakidhi vigezo katika soko la ajira.
“Dunia kwa sasa imeshakuwa Kijiji ndio maana tunasisitiza Digital Marketing kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi ili waende kukidhi vigezo sokoni ndio maana ukitoa mafunzo kwa wanafunzi wako wataweza kufungua mitandao yao ya kijamii vilevile kuanza kujitangaza hata kabla hawajahitimu na hilo ndio swala la muhimu zaidi”, amesema Dkt. Gillian Kasirye.
Dkt. Kasirye ameongeza kuwa SUA tayari kimeanza kupitia na kutengeneza Mitaala yao hivyo kupitia Mradi wa RUFORUM umewezesha kufanya kazi pamoja nao ili kuongeza nguvu kwa kile ambacho wamekwishafanya kwa kupita mitaala nakutengeneza utendaji kazi mzuri na kutoa uhakika wa wanafunzi kuweza, kupata elimu bora, kuongeza ushawishi kwa vijana na pia kukabiliana na soko la ajira
Aidha ameongeza
kuwa katika utoaji wa mafunzo ni muhimu kuzingatia soko linahitaji nini na hiyo
itawasaidia wao kama wakufunzi kuwafundisha wanafunzi wao kwa namna ya
kuwafanya kuwa bidhaa ili kuendana na ulimwengu wa sasa pia watategemea sana
kufanya yale waliojifunza darasani kwani watatumia uzoefu walioupata chuoni kutumia
teknolojia.
“Naiomba
Menejimenti yetu ya SUA iendelee kutuwezesha zaidi katika suala zima la Mafunzo
hivyo kama itawezekana tupate muda zaidi
wa kujifunza ili tuweze kupata mambo mengi zaidi na kwa wakati kwaajili ya
kuwafundisha wanafunzi wetu”, amesema Dkt. Wenaty
0 Comments