Na Gerald Lwomile.
Imeelezwa kuwa Hayati
Edward Moringe Sokoine, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati wa Utawala wa Awamu ya Kwanza iliyoongozwa na Hayati Mwl.
Julius Kambarage Nyerere alikuwa mtu aliyejua kutunza na kalinda Mazingira.
Akizungumza Aprili 12, 2024 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Misa ya Kumbukizi ya Miaka 40 ya Hayati Edward Sokoine iliyofanyika Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha. Balozi Joseph Sokoine ambaye ni
mtoto wa Hayati Edward Sokoine amesema ukiwa unaingia katika Kijiji cha Enguik,
Kata ya Monduli Juu utaona msitu mkubwa wa miti uliopandwa na
Hayati Edward Sokoine.
Amesema msitu huo umeshamiri
kijijini hapo umepandwa kwa akishirikiana na Chuo cha Misitu cha Olmotonyi
kilichoko wilayani Arusha, ambapo pamoja na miti ya kigeni lakini pia walipanda
miti ya asili katika eneo hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Misa ya Kumbukizi ya Miaka 40 ya Hayati Edward Sokoine |
Akizungumzia maisha
alioyoishi na wasaidizi wake, Balozi Joseph Sokoine amesema Hayati Edward
Moringe Sokoine alikuwa na huruma sana, kiasi kuwa inapofika mapumziko ya mwaka
ya sikukuu aliwataka wasaidizi wake kwenda kujumika na familia zao, naye alibaki
akijumuika na familia yake pamoja na kuwa na shughuli nyingi za kiserikali ambazo
alilazimika kuzifanyia nyumbani.
Amesema pamoja na kuwepo
msitu huyo, Hayati Sokoine pia alipanda maua mbalimbali ambayo yanapendezesha
nyumba yake iliyopo kijijini Enguik na huo umekuwa mfano bora kwa kizazi chake.
Kauli hiyo ya Balozi Joseph
Sokoine inathibitishwa na aliyekuwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine
Taaluma na Ushauri wa Kitalaamu Prof. Peter Gilla ambaye katika Mdahalo wa
Kumbukizi ya miaka 40 ya Hayati Sokoine uliofanyika Aprili 8, 2024 katika
Kampasi ya Edward Moringe Sokoine SUA alisema akiwa Chuo cha Misitu Olmotonyi na
wanafunzi wenzake walishiriki kupanda miti katika msitu uliopo Enguik wilayani
Monduli.
Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo SUA kilipewa jina la heshima la mwanasiasa huyo Hayati Edward Sokoine mwaka 1984, kabla ya hapo
kilikuwa ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1970
na kilianza na Vitivo vya Kilimo, Misitu na Tiba za Mifugo.
Picha chini ni viongozi mbalimbali kutoka Serikali, Taasisi na wananchi wakiwa katika Misa hiyo 👇
0 Comments