Na: Tatyana Celestine
Wanawake
mkoani Morogoro wametakiwa kutoyafumbia macho matendo ya ukatili kwa watoto
mkoani humo na kutoa taarifa katika madawati yanayoshughulikia masuala hayo ili
kukomesha vitendo hivyo.
Naye Mkuu wa Wilaya Morogoro Bi. Rebeca Msemwa amewaasa wanawake kujiepusha na mikopo maarufu kama kausha damu ambayo inawadumaza kiuchumi na badala yake wakope kwenye Taasisi za mikopo ambazo zinamjali mjasiliamali, mfanyabiashara na mteja kwa kutoza riba nafuu.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kumkomboa mwanamke kiuchumi na kuwa wanawake wanahitaji ukombozi wa kifikra na kuongeza elimu madhubuti kuhusiana na haki za wanawake kwani bado kuna wanawake hawajui haki zao.
Akizungumzia haki na stahiki za mwanamke Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro Bi. Susan Kihawa amesema kuwa wanawake wengine hawaamini kama wana uwezo wa kuomba talaka bali ni mwanaume pekee hivyo elimu ni muhimu kwa wanawake na itawasaidia kuwa na uelewa.
Naye Mkurugenzi
wa Unganisha Enveromental Consarvation Organization (UCO) Bi. Sophia Kalinga
amesema kuwa ni wazi serikali imefanya juhudi za kumuinua mwanamke kiuchumi
katika nyanja tofauti kama vile elimu bure na fursa mbalimbali.
0 Comments