Na: Adam Maruma
Vyuo zinavyotarajia kuanza ujenzi na
vinavyoendelea na ujenzi wa majengo mbalimbali kwa ufadhili wa Mradi wa
Mabadiliko ya Elimu ya Juu Kiuchumi , (HEET) vimetakiwa kuzingatia ujenzi utakaohimili athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ili
majengo hayo yatumika muda wote bila
vikwazo vyovyote pindi yatakapokamilika.
Baadhi washiriki wa Mkutano wa HEET wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo |
Hayo yamesemwa na Bw. Dickson Haule, ambae ni Msanifu majengo wa Mradi wa HEET Kitaifa, wakati
akitoa majumuisho ya mawasilisho ya taarifa ya maendeleo za utekelezaji wa mradi huo kutoka vyuo vyote
vinavyonufaika na mradi huo.
Bw. Haule amesema suala la
mabadiliko ya tabia ya nchi limekuwa tatizo katika maeneo mengi duniani ambapo
baadhi ya maeneo kumeshudiwa mafuriko makubwa, ukame uliokithiri na joto kali
hivyo majengo hayo lazima yawe na miundo mbinu itakayohimili changamoto hizo.
‘Sisi kwa
upande wetu kwenye ujenzi wa majengo haya tuzingatie athari hizi hivyo nawaomba
mzingatie hilo ili majengo haya yatakapokamilika yaweze kutumika bila
changamoto yoyote’’, amesema Haule.
Msanifu majengo wa Mradi wa HEET
Kitaifa ameongeza kuwa, eneo la umeme mbadala wa Sola nalo linatakiwa kuzingati
katika ujenzi huo kwani kutegemea umeme wa maji ni tatizo ambalo ni muendelezo
wa athari za ukame unaosabishwa na mabadiliko hayo ya Tabia ya nchi.
Ametaja eneo lingine linalotakiwa
kuangaliwa ni la uvunaji wa maji ya
mvua, na kusema katika majengo waliyokagua wamekuta uvunaji wa maji
umezingatiwa kwa kuweka mabomba ya kuvunia maji.
‘’Katika
baadhi ya maeneo tuliyotembelea tumeona majengo yenye miundombinu ya uvunaji maji
lakini hayajaonesha mahala pa kuhifadhi maji yaliyovunwa katika kipindi cha
mvua hivyo nawaomba mkaliangalie hilo hata kwa wale ambao hawanyaonesha kabisa
namna watakavyotekeleza miradi hiyo, wakafanye hivyo e’’ amesema Bw. Haule.
0 Comments