SUAMEDIA

SUA kuboresha vitendea kazi Idara ya Sayansi ya Udongo na Jiolojia

Na, Winfrida Nicolaus  na Tatyana Celestine

Maabara ya Sayansi ya Udongo, Idara ya Sayansi za Udongo na Jiolojia iliyopo Chuo Kikuu cha Sokoine imenunua na kukarabati vifaa vya upimaji udongo hivyo kuongeza uzalishaji katika sekta ya Kilimo.



Hayo yamebainisha na Mkuu wa Maabara ya Sayansi za Udongo kutoka Idara ya Sayansi za Udongo na Jiolojia SUA Amour  Suleimbapo amesema kupitia Mradi fedha zipatazo milioni 400 zimetolewa na Miradi ya Utafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Amesema mashine kubwa mbili ikiwemo Microwave Digestor pamoja na ICP OES (Inductively Coupled Plasma Optical Emission Spectroscopy)na kuweza kukarabati mashine yao kubwa ambayo imekuwa haifanyi kazi kwa muda mrefu iitwayo AAS (Atomic Absoption Spectiometer).

Amour Suleiman amesema wamebadilisha mfumo wa kieletroniki kwa maana ya kununua vifaa vya kieletroniki na programu wanazotumia katika usajili wa sampuli lakini pia upatikanaji wa data hivyo kuboresha mfumo mzima wa utoaji majibu na pia uhifadhi wa taarifa za wateja wao.

Bw. Suleiman amesema Microwave Digestor waliyonunua ina uwezo wa kuchakata sampuli ishirini na nne (24) kwa muda wa dakika 50 ambapo hapo awali walikuwa wakitumia mfumo wa Open System/Digest System ambao ulikuwa unawaruhusu kuchakata sampuli ishirini (20) kwa siku tatu.

‘‘Lakini pia kwenye hiyo mashine ambayo ni ICP OES mashine ambayo ni ya kisasa zaidi na tunafikiri ni Maabara nne tu ambazo zipo nchini kwetu aa kwenye kupima sampuli kwa haraka na inaweza kutavipengele ambavyo’’, amesema Amour Suleiman.

Aidha Mkuu huyo wa Maabara amesema kupitia Mradi huu vifaa hivyo tayari wamepita katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kilombero, Ruvuma-Madaba, Makete pamoja na Meatu na maeneo mengine kumekuwa na manufaa makubwa kwa wakulimayamekuwa makubwa.Aidha katika suala la umwagiliaji imekuwa msaada mkubwa kwa sababu wameweza kupima maji yanayopaswa kutumika kwa ajili ya umwagiliaji hivyo wanashauri mkulima kupima maji kabla ya matumizi ili kujua ubora wa maji hayo.

 ‘‘Maabara yetu kwa sasa imekuwa na ufanisi mkubwa zaidi ukilinganisha na awali hivyo nipende kuwakaribisha wadau mbalimbali wakiwemo wakulima wadogowadogo, wakati, wakubwa lakini pia makampuni kutumia maaba ajili ya upimaji wa sampuli, maji, mbolea na mimea kabla ya kuanza kuzitumia mashambani’’, ameeleza Amour Suleiman.       

Picha kutoka Maktaba





                               Unaweza angalia zaidi kupitia video kuhusiana na Sayansi ya Udongo  kupitia link hapa chini
https://vm.tiktok.com/ZMMYU2oKg/


Post a Comment

0 Comments