Na Gerald Lwomile
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan amewataka watendaji aliowateua
wakiwemo wakuu wa mikoa nchini wakiwemo aliowateua hivi karibu
kuhakikisha wanatatua migogoro ya ardhi iliyokithiri nchini.
Rais Samia amesema hayo katika Uapisho wa Viongozi Wateule
uliofanyika Ikulu Jiji Dar es Salaam ambapo ameshangazwa kuona pamajo na
viongozi kuwa katika maeneo hayo watu wanadhurumiwa ardhi huku baadhi ya
migogoro hiyo ikitokana na kauli za viongozi.
Akizungumzia namna ambayo Serikali ina mpango wa kupunguza
kukopa amewahimiza wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa mapato na
kuhakikisha wanavunja mitandao inayochepusha fedha.
Aidha Halmashauri inayokusanya kidogo itapata kulingana na
ukusanyaji wa mapato, migogoro ya ardhi imekuwa mengi kiasi kuwa watu hawana
furaha wanadhurumiwa ardhi na kuna migogoro mikubwa ya ardhi
Rais Samia amentaka Mkuu wa mpya wa Mkoa wa Mtwara Luteni
Kanali Patrick Sawala kuhakikisha
anadumisha ujirani mwema kati ya Tanzania na Msumbiji kwa kuwa na vikao vya
mara kwa mara ili kutatua changamoto na kuhakikisha uzalishaji wa za zao
la Korosho huku akitilia mkazo
uimarishaji wa kongani ya uchambuzi wa korosho ili kuliongezea thamani zao
hilo.
Akizungumzia mazao ya Tumbaku Asali na Pamba Mhe. Rais
amemtaka Mkuu wa Mkoa mpya wa Tabora Paul Chacha kuhakikisha anasimamia vizuri
mazao ya Tumbuku lakini pia kuhakikisha anpambana na changamoto ya ukataji miti
ovyo mkoani humo.
Awali akimkaribisha Mhe. Rais kuzungumza katika Uapisho huo
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi
bado kuna changamoto ambazo wakuu wa mikoa na wilaya wanapshwa kuhakikisha
wanazikabili na kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja kwa sababu wanajenga
nyumba moja na kama kuna na utengengano basi kazi zinazorota katika maeneo yao.
Viongozi wengine walioapishwa ni pamoja na Patrick Chongolo
kuwa mkuu mpa wa Mkoa wa Songwe, Luteni Kanali Patrick Sawala kuwa Mkuu mpya wa
Mkoa wa Mtwara na Paul Chacha kuwa mkuu mpya wa Mkoa wa Tabora
0 Comments