Na: Tatyana Celestine
Wakulima nchini wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya viuwatilifu kwa kujua kanuni bora za utumiaji, kuvitambua viuwatilifu vilivyosajiliwa kwa matumizi kwani wasipotumia vema watakumbana na changamoto na kutoona matokeo chanya waliotarajia.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa wakulima mkoani Iringa Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Mamlaka ya Afya za Mimea na Viuatilifu (TPHPA) Bw. Jumanne Rajabu amesema kuwa viuatilifu vyote nchini vinavyoruhusiwa kutumika lazima viwe vimesajiliwa kutokana na viuatilifu hivyo vimefanyiwa utafiti na kukubalika kwa matumizi na kupata matokeo mazuri kuliko kutumia viuwatilifu holela.
Aidha Bw. Rajabu amesema kuwa lengo lingine la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakullima ili kuweza kufahamu kanuni mbalimbali za ufanyaji biashara wa viuatilifu nchini kwani biashara hiyo inadhibitiwa na sheria na kanuni hivyo wanapaswa kufuata utaratibu uliowekwa na kuufanyia kazi hatimaye nchi iweze kuwa na wafanyabiashara weledi.
Nae Mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Maneno Chidege amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwa wakulima na wafanyabiashara kwa kuweza kutambua viumbe waaribifu na sumu sahihi ya kutumia kwani suala hili imekuja baada ya Tanzania hivi karibuni kuwa na changamoto ya magonjwa mbalimbali kwenye mazao hivyo bila kuwapatia ufahamu Mkulima au Afisa pembejeo wanaweza kutumia kiuatilifu kwa kiumbe ambaye hamjui na kufanya lengo kutotimia kutokana naina ya wadudu hao.
Kwa upande wake Mkulima Bw.Jason Mwalongo ambaye amehudhulia mafunzo hayo amedhihirisha kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwao kutokana na kuongeza uelewa wa vitu vipya kwani baina yao wapo wanaofanya na wanaojiandaa kufanya biashara za viuatilifu hivyo fursa hii imekuja kwa wakati muafaka kwani wataelewa makundi ya viuatilifu pamoja na kutambua namna bora ya kuwahudumia wakulima .
Nae Bi. Sarah Samson kutoka Kiesa mkoani Iringa amesema kuwa matumizi sahihi ya viuatilifu shambani yatafanyika vizuri pale mkulima atakapokuwa na uelewa ni sumu gani atumie, kwa wakati gani, na kiwango kipi kulingana na ugonjwa shambani hivyo mafunzo haya yatafanya mazao yao kukua kwa ubora zaidi.
ReplyForward |
0 Comments