Mkurugenzi wa Elimu ya Juu nchini, Prof.Peter Msoffe amewataka
watalaam kutoka vyuo na taasisi ya elimu ya juu kuzingatia miongozo
inayosimamia mradi wa HEET katika kutekeleza
shughuli zinazofanyika katika maeneo yao.
Prof. Msoffe ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye mkutano
uliowakutanisha watalaam hao amesema ni vyema mradi huo ukatekezwa
ipasavyo ikiwemo ujenzi wa madarasa na
ofisi zingine za kiutawala na kuwata kuongeza kasi ya usisamizi na utekelezaji
huo.
‘Ili Benki
ya Dunia iweze kuona umuhimu wa kuongeza fedha angalau mnufaika wa mradi awe
ametekeleza mradi kwa asilimia 40 hii itawaweka katika nafasi nzuri ya
kufikiriwa katika kuongezewa fedha hivyo inatakiwa kila mmoja ahakikishe
anaongeza kasi ya utekelezaji wa mradi’’
amesema Prof. Msoffe
Mkurugenzi huyo pia
amezitaka taasisi hizo, hadi kufikia mwezi wa 4 mwaka 2024 ziwe
zimefikia asilimia 50 ya utekelezaji wa mradi wa huo na kusema kutokana na
taarifa ziliwasilishwa na Taasisi hizo, nyingi zinatia moyo kwa hatua wanayoendelea
nayo.
‘’Nawakumbusha
washirika kuwatumia watalaam hawa wa HEET, ili mradi uendelee kuwa kwenye
malengo ya uanzishwaji wake endapo hamtawatumia hawatakua na kazi za kufanya na
pia si sahihi kabisa’’, ameongeza
Prof. Msoffe.
Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA), kimeungana na Vyuo na
Taasisi Zingine zaidi ya 10 za Umma zinazonufaika na Mradi wa Mabadiliko ya
Elimu ya Juu Kiuchumi, (HEET) kujadili mafanikio, na changamoto za miundo
mbinu inayotekelezwa kwa fedha za HEET
kwenye mkutano unaofanyika katika ukumbi mpya wa Makataba ya Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam.
Mradi wa HEET unafadhiliwa na Benki ya Dunia, ukitarajiwa
kufanya mabadiliko ya Kiuchumi kwenye Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa kuongeza madarasa,
ofisi za utawala, vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kupitia mitaala
mbalimbali ili iweze kufanyiwa mabadiliko na kuendana na mahitaji ya sasa ikiwa
kutakua na ulazima huo, na tayari mradi huu umetimiza miaka 2 tangu kuanza kwa
utekelezaji wake.
Vyuo vilivyoshiriki ni SUA.SUZA,UDSM,NELSON MANDELA nk.na kwa upande wa Taasisi ni HESLB.
0 Comments