SUAMEDIA

Wafugaji Samaki washauriwa kuweka kumbukumbu

 

Na: Tatyana Celestine

Imeshauriwa kuwa ili kupata tija katika ufugaji samaki ni muhimu kuweka kumbukumbu kuanzia mwanzo hadi samaki anapoingia sokoni ikiwa ni pamoja na kuchukua sampuli kwani itamsaidia mkulima kujua kiasi cha chakula kwa ajili ya Samaki wake pamoja na uzito wao.



Akizungumza na SUAFM Mtaalam wa Samaki kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw. Augustino Jacob amesema kuwa ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha Samaki wachache wanavuliwa kila mwezi na kupimwa uzito, hii itamsaidia mkulima kujua kasi ya ukuaji wa Samaki na kutambua kiasi sahihi cha chakula chake na wakati husika.

Aidha ameongeza kuwa uwekaji kumbukumbu za bwawa na kila kinachofanyika itampa mkulima urahisi wa kuweza kutatua changamoto yeyote inayoweza kutokea kama vile magonjwa na ulishaji usiofaa kwani takwimu zinazowekwa zitaonesha mtililiko wote wa ufugaji.

Amesema kumbukumbu hizo zinaweza kumsaidia mkulima kupata ushauri kulingana na mazingira ya ufugaji tangu alipoanza hadi mwisho tofauti na mkulima asiyeweka kumbukumbu kwani inakuwa ni vigumu mshauri kujua nini kifanyike

Pamoja na mambo mengine Bw. Augustino amesema kuwa kumbukumbu zinasaidia hata wakati wa uvunaji wa samaki kwani mkulima anajua gharama alizotumia na uhakika wa uzito wa Samaki anaowapeleka sokoni na hiyo itamletea tija.


Unaweza kuangalia namna bora ya ufugaji samaki kambale bofya hapa chini


 

Post a Comment

0 Comments