SUAMEDIA

Naibu Waziri Uchukuzi atembelea miundombinu ya reli iliyoharibiwa na mvua

 

Na: Josephine Mallango

Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amefanya ziara kutembelea reli ya kati kujionea hali ya uharibifu uliojitokeza baada ya mvua kubwa kunyesha kuanzia January 25 mwaka huu.


Mhe. Kihenzile amefanya ziara hiyo Jumapili Februari 4, 2024 katika eneo la Lukobe Manispaa ya Morogoro, Munisagara na Mzanganza wilayani  Kilosa na Gulwe iliyopo wilaya Mpwawa mkoani Dodoma ambapo ameambatana na Wataalamu kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Mhe. Kihenzile amejionea hali ya uharibifu wa reli ya kati uliosababishwa na maji kujaa na reli kusombwa na maji sehemu ya Mzanganza ambapo tayari mafundi wameanza kazi ya kurejesha miundombinu hiyo katika maeneo yote yaliyoathirika ili usafiri kupitia reli hiyo uweze kurudi baada ya kusitishwa tangu mwishoni mwa mwezi January, 2024.


Akiwa kwenye ziara hiyo Naibu waziri huyo amesema amefanya ziara ili kuangalia maeneo ya miundombinu ya reli yaliyoharibika kutokana na mvua na kukata mawasiliano ya reli yote ya kati hali ambayo imekuwa na  athari kubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla katika sekta ya uchumi na usafirshaji.

 Aidha Mhe. Kihenzile amelipongeza Shirika hilo kwa kuchukua hatua za haraka za kuanza matengenezo ambapo ametoa maelekezo kwa ajili ya kuchukua tafadhari zaidi ili kuepusha madhara mengine yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.


 




Post a Comment

0 Comments