Na: George Joseph
Wadau mbalimbali wa elimu
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameendelea kupitia na kufanya
mabadiliko ya mitaala ya elimu ya Chuo itakayotumika kwa ajili ya ufundishaji
wa masomo mbalimbali yanayotolewa na Chuo hapo.
Baadhi ya wadau wa elimu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) walioshiriki kupitia na kufanya mabadiliko ya mitaala ya elimu ya Chuo hicho |
Akizungumza katika mkutano huo
Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti inayoshughulika na masuala ya Stadi za
Awali Dkt. Damas Philip amesema lengo la
kufanya mapitio ni kuboresha kulingana na hali ya kiuchumi ili uendane na
maendeleo ya taifa na pia kuzalisha wahitimu ambao wanakua na stadi bora za
kufanya kazi kulingana na fani wanazo somea.
Nae Mwl. Lidya Bupilipili anayefanya
kazi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanafunzi ameongeza kuwa mapitio
ya maboresho hayo yatasaidia kuimarisha zaidi wahitimu kulingana na uhitaji wa
sasa katika jamii, na kuongeza kuwa masomo kama ya usuluhishaji wa migogoro
yatasaidia kutatua migogoro mbalimbali katika jamii wanazoenda kuzihudumia.
Ameongeza kuwa mtaala mpya pia
utamuwezesha mwanafunzi wa kila fani anayehitimu kuwa na uwezo wa kujiajiri mwenyewe kuliko kutegemea ajira Serikalini, hata hivyo amesema kuwa kwa wale
watakaotaka kupata kazi Serikalini na sekta binafsi watafanya vyema katika
ushindani kwenye soko la ajira.
Mapitio hayo ya mitaala yanayoendelea
SUA ni muendelezo wa shughuli za
uboreshaji wa elimu unaotekelezwa na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya
Kiuchumi (HEET) kwa miaka mitano na
kufadhiliwa na Benki ya Dunia.
0 Comments