Na: Calvin Edward Gwabara.
Wakulima Barani Afrika wameomba
Bioteknolojia ipewe nafasi na kujumuishwa kwenye menyu ya zana za kilimo
zilizopo ili waweze kuchagua kulingana na mahitaji badala ya kuwekewa
vipingamizi huku ikinufaisha wakulima kwenye nchi zingine.
Mkulima wa kiongozi wa Pamba ya Bt kutoka Kenya Bwana Daniel Magondu (Wa pili kutoka kushoto aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kwenye mjadala huo wa wakulima wa Afrika, Wengine ni wakulima wenzio kutoka nchi mbalimbali.
Ombi hilo limetolewa na wakulima
kutoka mataifa mbalimbali wanaoshiriki mkutano wa Kimataifa wa Teknolojia za
Kilimo Barani Afrika Jijini Nairobi wakati wa mjadala wa wakulima uliohusu
umuhimu wa kuwapa wakulima nafasi sahihi katika masuala yanayohusu kilimo.
Akizungumzia umuhimu huo Mkulima wa kiongozi wa Pamba ya Bt kutoka Kenya Bw. Daniel Magondu amesema wanapata changamoto kubwa ya kufikia teknolojia zenye za kisasa na pembejeo zingine hali ambayo inawafanya washindwe kuzalisha kwa tija.
“Huwa najiuliza sana kama kuna teknolojia ambayo inakinzana na wadudu, Mabadiliko ya tabia nchi na magonjwa kwanini nashea jasho langu na visumbufu hivyo vya mazao? Lakini jibu likawa ni zuio la Serikali kwa wakulima kutumia mbegu hizo za zinazotokana na uhandisi jeni” Alieleza Bwana Fatch.
Aidha
amesema kuwa wakati wakulima wa nchi zingine duniani wanafaidi matunda ya
Sayansi na teknolojia kwenye matumizi ya mbegu hizo wakulima wengine
wanaendelea kuteseka na changamoto hizo za kilimo na kuwafanya washindwe kupiga
hatua na kuona kilimo ni mateso.
0 Comments