Na: Calvin Gwabara - Nairobi
Ongezeko
kubwa la ukuaji wa vijana ambao ni nguvukazi katika kufufua uchumi wa Bara la Afrika
hakujatumika vilivyo hali inayotokana na vijana kutoshirikishwa ipasavyo katika
shughuli za kilimo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Teknolojia za Kilimo Africa (AATF) Dkt. Canisius Kanangi wakati akitoa utambulisho kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Teknolojia za Kilimo Africa (ACAT) jijini Nairobi.
“Hali
hii inapelekea Bara la Afrika likihangaika kulisha watu wake na hivyo kuwa muagizaji
mkubwa wa chakula kwa ajili ya watu ijapokuwa ina ardhi kubwa yenye rutuba Duniani”alisema
Dkt.Kanangi.
Aidha
amesema kuwa AATF inaaamini katika matumizi ya Sayansi, teknolojia na ubunifu hasa
kupitia shuhuda kutoka kwenye nchi zaidi ya 24 za Afrika ambazo wamekuwa wakifanyakazi
na Serikali na Taasisi za utafiti za nchi hizo katika kuwaelekeza wakulima kuboresha
kilimo chao.
Akizungumza
kwenye mjadala wa kwanza iliyoangalia uwezeshwaji wa wakulima kuhimili changamoto
za kilimo kwa kutumia Sayansi Teknolojia na Ubunifu, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt.Amos Nungu amesema Tanzania ikombele katika kusaidia
idadi kubwa ya vijana nchini kushiriki kwenye kilimo cha kisasa na kujiletea maendeleo.
“Tanzania
inatambua nguvu ya vijana ndio maana imeanzisha programya (Building a Better Tomorrow)
kwa lengo kuwapa mazingira rafiki ya kufanya kilimo kwa kuwapatia miundombinu na
mitaji ili waweze kushiriki katika kujiletea
maendeleona kujenga taifa” alifafanua Dkt.Nungu.
Ameongeza
kuwa Serikali kupitia COSTECH imekuwa ikitoa fedha kuwezesha watafiti na wabunifu
kufanyiakazi bunifu mbalimbali zenye tija ilikuhakikisha Sayansi, Teknolojia na
Ubunifu unatumiwa na kusaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii na kuwapatia
kipato lakini pia tayari kuna makampuni machanga (startups) yanayotoa huduma katika
masuala ya kilimo.
Mkurugenzi
huyo amewaambia wadau wa mkutano huo mkubwa
wateknolojia za Kilimo Afrika kuwa COSTECH kama mshauri mkuu wa Serikali kwenye
masuala hayo wamewezesha kufanyika kwa tafiti
nyingi zenye tija kwa taifa ikiwemo Utafiti wa Mradi wa Mahindi yanayotumia maji
kwa ufanisi Afrika (WEMA) ambao umesaidia kupatika na kwa ina 11 za mbegu ambazo
zinatumiwa na wakulima nchini Tanzania.
Kwenye
mkutano huo mkubwa wa Teknolojia za Kilimo Barani Afrika unaofanyika Nchni Kenya
na kukutanisha wadau kutoka Afrika na duniani kote, Tanzania imewakilishwa
na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia ambaye ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Kilimo na Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Rais wa Zamani wa Nigeria Mhe. Dkt. Dr. Goodluck
Jonathan akifuatilia mawasilisho na mijadala kwenye Mkutano huo. |
0 Comments