Na Winfrida Nicolaus
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesaini Mkataba wa kupata Mtaalam wa Ushauri wa Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu na Kampuni ya Crystal Consultancy katika Kampasi ya Mizengo Pinda Mkoani Katavi kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Zoezi hilo limefanyika katika Kampasi ya Edward Moringe Sokoine mkoani Morogoro ambapo limeongozwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Utawala na Fedha SUA Prof. Amandus Muhairwa kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Raphael Chibunda.
Akizungumza na SUA Media Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Ununuzi na Ugavi SUA Kuruthum Abdallah Ndope amesema kampuni hiyo itaenda kusimamia majengo yanayotarajiwa kujengwa katika Kampasi ya Mizengo Pinda ikiwemo Hosteli, Cafeteria pamoja na Jengo la Utawala.
“Chuo kitaenda kunufaika kwa sababu miundombinu itaenda kuboresha na itasaidia katika kuongeza ufanisi mkubwa wa Chuo, udahili wa wanafunzi utaongezeka na kuleta manufaa makubwa kwa Chuo”, amesema Kuruthum Ndope.
0 Comments