SUAMEDIA

SUA yaanza kupokea wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2023/2024


Na: Winfrida Nicolaus

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Octoba 23, 2023 kimeanza kupokea Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo Chuoni hapo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 tayari kwa kuanza masomo.

Akizungumza na SUA Media wakati wa zoezi la mapokezi ya wanafunzi hao Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo Mikoani mjini Morogoro (Msamvu)  Bw. Philipo Lusotola Waziri Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi SUA ambaye ndiye Kiongozi wa mapokezi hayo amesema imekuwa ni furaha kubwa kwao kuendelea kuwapokea vijana kutoka maeneo mbalimbali  kwa kutumia ofisi yao ya muda kwenye Stendi hiyo ya Mabasi.

Amesema wapo katika eneo hilo kuhakikisha wanafunzi hao wapya wanakuwa salama wao pamoja na mali zao vilevile kuhakikisha wanafika sehemu husika kwa wakati bila usumbufu wowote hivyo kupitia Ofisi ya muda ambayo inafanya kazi kuanzia asubuhi mpaka muda wa saa nne usiku ipo tayari kwaajili ya mapokezi na kuwaondoa shaka wanafunzi wote ambao bado hawajawasili Chuoni na ni mara yao ya kwanza kufika Mkoani Morogoro kutokuwa na shaka .

“Licha ya kuwa na Ofisi yetu ya muda hapa stendi pia tunalo basi letu la Chuo ambalo kazi yake ni kuwakusanya wanafunzi wapya wanaokuja kujiunga na SUA toka maeneo mbalimbali na kuwafikisha sehemu husika ndio maana gari yoyote inayoingia stendi sisi tunakuwa wa kwanza kulifuata na kuuliza endapo kuna mwanafunzi wa SUA tunamchukua na kumuepushia usumbufu”, alisema Philipo Lusotola 

Kwa upande wake Gloria Tembo mmoja wa wanafunzi wapya waliochagulia kujiunga na SUA kwa mwaka wa masomo 2023/2024 kutoka Mkoani Ruvuma Wilayani Songea amesema amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata kutoa SUA ikiwa ni mara yake ya kwanza kufika mkoani Morogoro imekuwa rahisi kwake kufika sehemu husika bila usumbufu na kumfanya ajihisi mwenyeji.

Amesema SUA ni chaguo lake la kwanza kwakuwa mara zote amekuwa akikipenda Chuo hicho kwakuwa kimekuwa kwenye ndoto zake zaidi kutokana na taarifa zake nzuri ambazo amekuwa akizisikia hasa utoaji wa Elimu kwa njia ya vitendo unaomsaidia mwanafunzi kutoka chuoni hapo akiwa na ajira tayari mkononi mwake na si kusubiri kuajiriwa.

Naye Felishian Mutta kutoka Dar es Salaam amesema utaratibu wa mapokezi mazuri aliyoyapata kutoka SUA yamemfanya kukipenda zaidi Chuo hicho ambacho amekuwa akisikia taarifa zake za kuvutia kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki hasa kutoka kwa watu ambao wamesoma na kuhitimu Chuoni hapo hivyo ametoa wito kwa wale ambao bado hawajafika kuondoa shaka na anaimani kuwa watafurahishwa pia na mapokezi hayo.

Zoezi hilo la mapokezi likiambatana na zoezi la usajiri wa wanafunzi hao wapya kwa mwaka wa masomo 2023/2024 litaendelea wiki hii yote kabla ya kufanyika kwa siku ya kuyajua mazingira ya Chuo (Orientation)  Chuoni hapo. 






Post a Comment

0 Comments