Na :Asifiwe Mbembela
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),
Prof. Raphael Chibunda amewataka watumishi wa Kampasi ya Mizengo Pinda
kushirikiana kiutendaji wakati wa kutimiza majukumu mbalimbali ya kiutumishi wa
umma.
Prof. Chibunda ametoa wito huo kwa watumishi wa Kampasi ya Mizengo Pinda wakati wa ziara maalum aliyoifanya katika Kampasi hiyo akiwa ameambatana na Menejimenti ya Chuo kwa ajili ya kuwaeleza watumishi hao mipango ya Chuo kwa mwaka ujao wa masomo pamoja na kusikiliza na kutatua kero za watumishi wa Kampasi hiyo.
Prof.
Chibunda amewataka Watumishi wa Kampasi ya Mizengo Pinda kushirikiana katika
kazi na kuendeleza utamaduni wa SUA kuwa mfano wa kuigwa kwa Jamii inayowazunguka.
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Mipango, Fedha na Utawala Prof. Amandus Muhairwa
amewahimiza watumishi wa Kampasi hiyo kutosita kufika katika ofisi yoyote pindi
wanapokuwa na changamoto yoyote kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, akiwataka
kuacha tabia ya kuziogopa ofisi.
Kwa
Upande mwingine Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa
Kitaalamu Prof. Maulid Mwatawala amewakumbusha Wanataaluma kuzingatia misingi
ya ufundishaji kwa kufuata Utamaduni, Utaratibu na Mwongozo wa Chuo ili SUA
iendelea kuwa kitovu cha kuzalisha wanataalamu wenye tija kwa taifa.
Prof.
Mwatawala ameongeza kuwa Chuo kipo katika zoezi la kuboresha mtaala wa Chuo,
ambapo Kampasi ya Mizengo Pinda wamelenga kuongeza baadhi ya program ambazo
zitaongeza idadi ya wanafunzi watakaosoma katika Kampasi hiyo suala ambalo
litakuwa chachu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa jamii inayozunguka
Chuo na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
Dkt.
Winfred Mbungu, Mratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi
(HEET), akielezea maendeleo ya mradi huo kwa Kampasi ya Mizengo Pinda ambayo
itanufaika na ujenzi wa majengo matatu ya kisasa, amesema Mradi huo utakamilika
katika kipindi kilichokusudiwa.
Dkt.
Mbungu amesema mradi huo unadhamini mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu ambapo
amewasihi watumishi wa Kampasi ya Mizengo Pinda kutumia fursa hiyo kujiendeleza
kielimu, huku akibainisha baadhi ya watumishi waliopata udhamini wa kielimu
kupitia Mradi huo.
Menejimenti
ya Chuo imefanya ziara hiyo ikiwa ni mwendelezo wa kufanya ziara ya
kuwatembelea watumishi wa SUA katika Kampasi, Ndaki na Shule zao, ili kuwaeleza
mipango ya Chuo kuelekea mwaka ujao wa masomo pamoja na kusikiliza na kutatua
changamoto zinazowakabili watumishi hao.
0 Comments