Na : Asifiwe Mbembela
Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepanga kuanza kuendesha mafunzo tarajali na
kutoa ujuzi wa kilimo biashara kwa vijana ili kuweza kuunga mkono juhudi za
Wizara ya Kilimo katika kuinua kilimo kupitia
Mradi wa Building a Better Tomorrow
(BBT), unaotekelezwa hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Maulid Mwatawala aliposhiriki kikao kazi cha Wizara ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa mwishoni mwa wiki iliyopita alipokutana na Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Umma nchini.
Katika
kikao hicho upande wa Wizara imewakilishwa na Mratibu wa Mradi wa BBT Bi. Vumilia
Zikankuba na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara Bi. Tagie Daisy huku upande wa
Chuo mbali na Prof. Mwatawala pia alishiriki Kaimu Mkurugenzi wa Shahada za
Awali Dkt. Alex Matofali.
Akiongea
katika kikao hicho, Prof. Mwatawala ameahidi kuwa SUA itatoa ushirikiano kwa
Wizara kupitia nyanja mbalimbali za kilimo ili kuona vijana wengi zaidi
wananufaika na mpango huo kabambe wa kilimo hapa nchini.
"SUA
tutashirikiana na Wizara ya Kilimo katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuanzisha kituo cha BBT kwenye Kampasi za SUA; pia tutakuwa tunaendesha mafunzo
ya kilimo biashara, mafunzo tarajali na tunakusudia kuongeza uwezo wa kuandika
maandiko ya kutafuta rasilimali fedha na watu”, amesema Prof. Mwatawala.
Aidha,
ameongeza kuwa Chuo kwa kushirikiana na Wizara kitajikita katika kupima aina za
udongo na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu namna bora ya umwagiliaji ili
vijana waweze kunufaika na kilimo kwa kulima kisasa.
0 Comments