Na:
Winifrida Nicolaus
Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) katika utekelezaji wa maeneo saba ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) kimezindua Magari matatu, mawili aina ya Double Cabin na moja aina ya Land
Cruiser Hardtop kwa lengo la kusaidia kurahisisha shughuli za mradi huo
kwa ufanisi mkubwa ikiwemo ufuatiliaji wa masuala ya ujenzi.
Amesema wamekuwa na shughuli
nyingi ambapo zingine zitaanza hivi karibuni hasa za kufuatilia mambo mengi ya
ujenzi ambapo wamekuwa wakihitaji usafiri na mara nyingi wamekuwa wakitumia
magari ambayo yamekuwa na shughuli zingine Chuoni hapo hivyo magari hayo
yaliyozinduliwa yatarahisisha kazi kwa sababu ni mahususi zaidi kwaajili ya utekelezaji
wa shughuli za Mradi.
Dkt. Mbungu amesema wanatoa shukrani
kwa Fedha hizo walizozipata kupitia Mradi wa HEET pamoja na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia ambazo zimewezesha kupelekwa SUA na pia kuwezesha kununua
hayo magari ambapo wanatumaini yataboresha Mazingira ya watu kujifunzia pamoja
na kufundishia na pia kuboresha kiwango cha wahitimu wao ambao watamaliza SUA.
“Hii
ni seti moja wapo lakini tuna magari mengine tunayatarajia hapo baadae ambayo
yatakuwa zaidi mengine ni kwa Mafunzo kwa vitendo zaidi kwa maana ya mabasi
pamoja na minbus kwaajili ya
kurahisisha shughuli za mafunzo kwa vitendo lakini haya tuliyoyazindua ni zaidi
kwaajili ya kufanikisha shughuli za kukimbia kufuatilia utekelezaji wa Mradi
amesema”, Dkt. Mbungu.
Aidha Dkt. Mbungu ametoa wito kwa wadau wote wakiwemo
watekelezaji wa Mradi ambao ni Chuo kizima kwa ujumla kuwa washirikiane ili
kuweza kutekeleza malengo ya Mradi ambao upo mahususi kwaajili ya kuinua
shughuli za kitaaluma ikiwemi uboreshaji wa Mitaala, programu mbalimbali Chuoni
hapo lakini pia Miundo mbinu wezeshi kwaajili kujifunzia na kufundishia ili
ifikapo mwaka 2025/2026 kuwepo na mabadiliko yenye tija.
0 Comments