Na: Calvin Gwabara - Tanga.
Watafiti wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na watafiti kutoka Mamlaka ya Afya ya
Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) wanafanya majaribio ya matumzi ya wadudu
rafiki kupambana na Viwavijeshi vamizi kwenye mahindi.
Akizungumza na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mradi huo wa Utafiti Prof. Gration Rwegasira kutoka SUA amesema baada
ya utafiti na majaribio ya maabara na baadae ngazi ya kitalu nyumba wamebaini
kuwa wadudu aina ya Trichogramma mwanzae
na Telenomous remus wameonesha uwezo
mkubwa katika kupambana na viwavijeshi vamizi.
‘’Katika utafiti wetu tukabaini
wadudu hao aina mbili ambao ni nyigu wadogo sana wenye uwezo wa kuwadhibiti
Viwavijeshi vamizi na wao wanauwezo wa kushambulia mayai ya kiwavijeshi na sio
kiwavijeshi mwenyewe na hivyo kwakuwa wanashambulia mayai yao wanasababisha
kutoongezeka na kupotea kwa viwavijeshi kwa kuwa hawazaliani shambani‘’alieleza
Prof. Rwegasira.
Aliongeza ‘’Kwa kuwa tunatambua
hatua ambayo inaathiri zaidi mazao ya wakulima ni Kiwavi kwa hiyo mayai
yasipoanguliwa maana yake kiwavi hatoanguliwa na hivyo kuwa tumemsaidia mkulima
kumaliza wadudu hao hatari kwenye mazao ya mkulima bila kutumia viuatilifu
ambavyo vina sumu‘’.
Prof. Rwegasira amesema hivi sasa
wapo katika hatua ya tatu ambayo ni kuwapandikiza wadudu hao kwenye mashamba ya
wakulima yaliyolimwa Mahindi kwenye Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro na Muheza
mkoani Tanga ili kuona namna ambavyo wanafanya kazi kwenye mashamba halisi
yenye wadudu aina ya Viwavijeshi Vamizi.
‘’Leo tumeweka kwenye mashamba
haya lakini tutarudi kuweka tena baada ya wiki mbili na hii inatakiwa ifanyike
mahindi yakishafikisha wiki tatu hadi nne baada ya kupandwa maana majani
yatakuwa matatu hadi manne na ndio wakati ambao Viwavijeshi Vamizi wanakuja kutaga
mayai yao kwenye mimea kwa hiyo wakifika na kutaga wadudu hao rafiki
wanashambulia mayai yote shambani”, alieleza Prof. Rwegasira.
Aidha amesema wadudu hao rafiki
wanatumia mayai ya Viwavijeshi Vamizi kuweza kuzaana hivyo ndio maana
wanayatafuta mayai hayo na kudunga sindano na kuweka mayai yao ndani ya yai la
kiwavijeshi vamizi na kwa namna hiyo wanamaliza kizazi cha Viwavijeshi vamizi
kwenye shamba la mkulima na kubaki wao ambao hawana madhara.
Amesema utafiti huu ukikamilika
utawasaidia wakulima kuondokana na matumizi ysiyofaa ya viuatilifu vyenye
viambata sumu ambavyo ni hatari kwa afya zao na mazingira na zaidi sana hawa
wadudu rafiki watampunguzia Mkulima gharama za uzalishaji mazao ya chakula hasa
mahindi na kuleta tija kwenye kipato cha kaya na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkulima Salehe
Alfan Ally mkazi wa Dumila Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amepongeza utafiti
huo ambao utasaidia kulinda mazao yao kwa kuwa matumizi ya madawa wengi
hawayawezi maana ni ghari na mwisho wa siku wanapata hasara wakati wa kuvuna.
‘’Awali tulizoea kulima mahindi
bila kupulizia dawa tukawa tunapulizia dawa kwenye mashamba ya nyanya tu lakini
toka mwaka 2017 walipokuja wadudu hawa Viwavijeshi Vamizi hali ya maisha yetu
yamekuwa magumu tunapata hasara maana sio wote wanamudu kununua madawa
kupulizia kila baada ya wiki mbili hadi tunapovuna na bado hawatoweki‘’
alieleza Bw. Salehe.
Aliongeza kuwa ‘’Yani inafika mahali tunaamua
tu kuacha wadudu wale na kile kinachobaki ndicho tunachopeleka nyumbani kama
mavuno ya mwaka na unakuta muda mwingine unapata gunia moja au mbili kwenye
shamba la mahindi la ekari moja na unakuta mahindi yenyewe ni yale madogo madogo
sana ambayo yameliwa hadi magunzi yamejikunja‘’.
Nae Afisa Kilimo Mwandamizi kutoka
Kata ya Mlingano wilayani Muheza mkoani Tanga Bw. Jimmy Mhina amewapongeza
watafiti hao wa SUA na TPHPA kwa kuja na ubunifu huo wa matumizi ya wadudu
rafiki katika kukabiliana na Viwavijeshi Vamizi na kuomba jitihada hizo za
majaribio zifanikiwe kwenye mashamba ili kumtua mkulima mzigo wa hasara
zinazosababishwa na wadudu hao hatari kwenye mazao.
‘’Wakulima wengi wanashindwa
kununua mfano mbolea na hata mbegu bora sasa ujio wa wadudu hawa unawalazimisha
gharama ya kununua Viuatilifu ambavyo ni ghali na hivyo wengi wao hawapigi dawa
wanahudumia shamba na kusubiri kile watakachobakisha wadudu hao ndio apeleke
kwenye familia kwa kweli wanapata tabu na kuongeza umasikini kwa wakulima wetu‘’
alifafanua bw. Mhina.
Viwavijeshi Vamizi kutoka Amerika
viliingia nchini mwaka 2017 kwenye mikoa michache lakini kufikia mwaka 2019
viliripotiwa kwenye mikoa yote ya Tanzania na kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) ambao ndio wafadhili wa utafiti huo wanasema
Viwavijeshi Vamizi wanauwezo wa kushambulia mazao zaidi ya 80.

Mdudu rafiki aina ya Telenomus remus,akitoboa na kutaga mayai yake kwenye mayai ya Kiwavijeshi Vamizi. |
Mdudu rafiki aina ya Trichogramma mwanzae akitoboa na kutaga mayai yake kwenye mayai ya Kiwavijeshi Vamizi. |
Mtafifti Mkuu kutoka SUA Prof.Gratian Rwegasira na wataalamu kutoka TPHPA wakiwa kwenye zoezi la kuweka wadudu hao rafiki kwenye mashamba ya wakulima. |
Picha ya karibu ya namna Kiwavijeshi vamzi anavyoshambulia zao la Mahindi. |
Sehemu ya mashamba ya Mahindi ya wakulima Wilayani Mvomero yaliyoathiriwa na Viwavijeshi Vamizi. |
Sehemu ya picha anayoonesha wadudu hao rafiki wakiwa kwenye maabara kwenye Maabara za TPHPA kibaha. |
0 Comments