Na: Farida Mkongwe
Serikali imekipongeza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kufanya kazi nzuri ya kuendeleza kilimo nchini na kuwataka watanzania kutumia fursa zinazozalishwa na Chuo hicho ili kupata maarifa makubwa zaidi ambayo yatawasaidia kupata maendeleo na kujikwamua na umaskini.
“Kubwa zaidi ni kwa watanzania waweze kuona
fursa hizi zilizopo katika Maonesho haya, natamani sana watanzania wanaokuja
waweze kupita mabanda yote lakini wafike SUA hapa ndipo watapata vitu vingi
zaidi, watapata maarifa lakini wengine wataona hata watoto wao wanaowazaa wapi
pa kuwapeleka wakapate maarifa zaidi”, amesema Mh. Jafo.
“Maonesho haya yaNanenane nyie ndio mmeyabeba, dhana
ya kilimo ndio inapatikana hapa, kwa sababu mbinu za kilimo na tafiti zote zipo
kwenu kwa hiyo niwapongeze sana naona SUA
sasa imekuwa sana sio SUA ya wakati ule maana wakati ule hata Idara zilikuwa
chache sana, Mkuu wa Chuo nikupongeze sana kwa sababu uongozi wako nao
umesaidia kuleta maendeleo katika mambo mengi sana.
Waziri Jafo amesema Serikali ya
Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza sana kwenye Sekta ya Kilimo,
Mifugo na Uuvuvi ambapo hata kwenye
bajeti Rais Samia amefanya mabadiliko na kuongeza bajeti kutoka sh.Bilioni 294.2
kwa mwaka 2021/2022 hadi kufikia sh. Bilioni 970.8 kwa mwaka 2023/2024 na
kusema kuwa bajeti hiyo ni mapinduzi makubwa yenye kulenga kuleta mabadiliko
chanya katika kilimo.
Waziri Jafo amesema katika
kipindi hiki ambapo Rais anafanya uwekezaji huo SUA ina nafasi kubwa sana ya
kuwasaidia wakulima kwa sababu ina Teknolojia zote za kisasa na Wataalamu wa
kutosha wa kuendeleza kilimo cha Tanzania.
Awali wakati Waziri Jafo
akitembelea banda hilo la SUA Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda
alimweleza waziri huyo shughuli mbalimbali za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambazo
zinafanywa na SUA kupitia Mabanda yaliyopo kwenye Maonesho hayo ya ya 30 ya
Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Mashariki.
Picha mbalimbali za Waziri Suleiman Jafo akitembelea Banda la SUA
0 Comments