Na: Farida Mkongwe
Watanzania wametakiwa kutumia
zaidi dawa za asili zinazotokana na miti dawa ambazo zimethibitishwa na Shirika
la Viwango Nchini (TBS) kwa sababu dawa hizo za asili hutumika kama chakula
tofauti na dawa nyingine ambazo ukizitumia kwa muda mrefu zinatengeneza usugu
mwilini na hivyo hata ukiugua inakuwa ni vigumu kupona kwa kutumia dawa hizo.
Wito huo umetolewa Julai 20, 2023 na Fundi Maabara kutoka Idara ya Kemia na Fizikia katika Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bi. Aneth Coster wakati akizungumza na SUAMEDIA katika viwanja vya Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika Mnazi Mmoja jijini Dar Es Salaam kuhusu dawa za asili zinazotengenezwa na Idara hiyo.
Bi. Aneth amezitaja dawa
zilizopo katika maonesho hayo kuwa ni Synadol
ambayo inatibu mafua makali, kifua, pumu na mafindofindo ambayo imetengenezwa
kwa kutumia mti dawa baada ya kufanyiwa tafiti za kutosha na kubaini mti huo
una uwezo wa kutibu magonjwa hayo.
“Pia tuna dawa nyingine inayotibu
ngozi ambayo ipo katika mfumo wa sabuni na imetengenezwa kwa kutumia mti dawa unaoitwa
Mvunja kongwa ambao kitaalamu unalikana kwa jina la Synadenium na majani yake nayo yamefanyiwa tafiti na kuona yanatibu
kwa hiyo sabuni hizi zimetengenezwa kwa kutumia majani na mizizi na zinatibu
ngozi kama imeathirika na fangasi”, amesema Bi. Aneth.
Dawa nyingine ambazo
zimetengenezwa na Idara hiyo ya Kemia na Fizikia ni dawa ya kusafisha na
kungarishia sinki la chooni hasa likiwa na uchafu korofi, pamoja na vitasa
mikono (sanitizer).
“Tafiti zinaendelea na pia tuna
kitu kinaitwa indicator (viashiria) hivi
vinatumika kwenye kuweza kuchanganya tindikali mbili base na acid ili upate neutralization yaani upate end point kwa hiyo tuna indicator ile ambayo imetengenzwa kwa
miti nia yetu kubwa ni kwamba badala ya kuendelea kutumia indicator ambazo tunazinunua toka nje tufike mahala tutumie bidhaa
zetu za ndani ili kupunguza gharama”, amesema Bi. Aneth.
Baadhi ya dawa, sabuni na vitakasa mikono vinavyotokana na miti ya asili. Picha na Asifiwe Mbembela |
0 Comments