Na: Farida Mkongwe
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Kituo cha Kusini mwa Afrika cha Uchunguzi wa Magonjwa Yanayoambukiza (SACIDS) kimefanikiwa kutumia kinga ya
ngamia kwa ajili ya kutengeneza vifaa tiba, chanjo na dawa za kutibu magonjwa
mbalimbali yanayowapata binadamu, wanyama na mimea.
Mhadhiri wa SUA wa Idara ya Fiziolojia, Biokemia na Famakolojia ambaye ni Mtafiti kutoka SACIDS Dkt. Edson Kinimi akizungumzia kuhusu kinga ya ngamia. Picha na Asifiwe Mbembela. |
“Na hii teknolojia sasa tunataka tuanze kuifundisha kwenye
Vyuo vikuu vyetu kwa ajili ya kutumia ngamia kutengeneza hizo kinga zenye uwezo
wa kuua vijidudu vya magonjwa ndani ya miili ya wanyama na binadamu, hizi kinga
za ngamia zinaweza kutumika kutengeneza hata dawa za kuzuia kansa”, amesema
Mhadhiri huyo.
“Mojawapo ya kinga ya ngamia ambayo imeshatengenezwa kule Ulaya
imeweza kusaidia kuzuia magonjwa ya kuganda kwa damu kwa binadamu, sasa sisi kama kituo cha Umahiri cha Utafiti, SACIDS
ambacho kipo chini ya SUA tumejikita kutumia kinga hii ya ngamia kutengeneza vifaa vya
kutambua magonjwa kwenye jamii kwa haraka sana”, amesema Dkt. Kinimi.
Amesema hadi sasa kwa Tanzania wamezalisha kinga za ngamia
tisa zenye uwezo wa kukabiliana na ugonjwa wa sotoka ya mbuzi na kondoo na kinga hizi sasa zinaweza kutumika kwenye
magonjwa ya binadamu, wanyama na mimea.
“Kwa sasa tunazo kinga tisa ambazo zimeonesha uwezo mkubwa wa
kutambua virusi vya sotoka ya mbuzi na kondoo na huu ni mwanzo mzuri wa
kuendeleza hii kinga katika nyanja nyingine za maradhi hata sumu kwa mfano mtu
anaweza kuwa ameng’atwa na nyoka tunaweza kutengeneza vipande vya kinga ya
ngamia vya kuzuia ile sumu ya nyoka isimdhuru binadamu”, amesema Dkt. Kinimi.
0 Comments