SUAMEDIA

SUA yaja na mpango wa kubuni Vazi la Taifa

Na Winfrida Nicolaus

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Ndaki ya Kilimo, Idara ya Lishe na Sayansi ya Mraji inayotoa Mafuzo kwa Vitendo katika fani ya Ubunifu na Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali (Costume Designing Construction) wanaamini wataweza kutoa Mbunifu wa Vazi la Taifa au wazo litakalotoka Chuoni hapo kupitia wanafunzi wao na kutumiwa na wabunifu wakubwa nchini katika kutengeneza vazi hilo litakalomtambulisha Mtanzania.


Bi. Zahra Majiri Mhadhiri kutoka SUA kwenye Idara ya Sayansi ya Mlaji na Lishe akizungumza mara baada ya Maonesho ya Bunifu za Mavazi ya aina mbalimbali ikiwemo Vazi la Taifa.

Amebainisha hayo Bi. Zahra Majiri Mhadhiri kutoka SUA kwenye Idara ya Sayansi ya Mlaji na Lishe wakati wa Maonesho ya Bunifu za Mavazi ya aina mbalimbali ikiwemo Vazi la Taifa, Makabila mbalimbali nchini Tanzania pamoja na Mavazi ya kuvaa katika shughuli mbalimbali yaliyofanywa na wanafunzi wa Mwaka wa pili na wa tatu wa kozi ya Sayansi ya Mlaji na Kaya Chuoni hapo katika Kampasi ya Edward Moringe Sokoine mjini Morogoro.

Amesema katika miaka takribani mitano wanafunzi wao wamekuwa wakibuni na kuonesha mavazi ya kiasili ya Tanzania lakini pia nje ya Tanzania na mwaka huu 2023 wameweza kubuni Vazi la Taifa ambapo muelekeo umekuwa mzuri hivyo wanaimani wanafunzi hao wakiweza kupewa Maarifa zaidi kutokana na Ujuzi wanaoupata Chuoni hapo, wakichanganya na wanaoupata kwenye maeneo mengine uhakika wa Vazi la Taifa kutoka SUA ni mkubwa.

“Hii ni sehemu ya somo sio kama walivyozoea kuita Fashion Show na somo hilo linaitwa Caltural Aspect of Clothing, somo lingine ni Costume designing and construction na masomo hayo yote asilimia 80 ni kwa vitendo na 20 inabaki kwenye nadharia hivyo wanafunzi wetu huwa wanapewa mandhari mbalimbali zinazohusiana na mada mbalimbali ambazo zimefundishwa darasani na baadae kubuni mavazi kulingana na mandhari walizopewa”, amesema Bi.Zahra Majiri

Kwa upande wake Bw. Valentino Esau Mwinuka Mtaalam wa Nguo na Mavazi na Mhadhiri Msaidizi SUA ambaye alikuwa mmoja wa majaji katika maonesho hayo amesema mahali ambapo SUA imefikia kuna uwezekano mkubwa Mbunifu wa Vazi la Taifa kutokea chuoni hapo kwa sababu kupitia maonesho hayo ya bunifu imeonesha kabisa kuna mwanga wa kupata mbunifu huyo vilevile wapi wanaelekea katika suala zima la bunifu za mavazi.

Amesema Vijana wamejitahidi kubuni Mavazi katika maeneo mbalimbali ambayo walitakiwa kuyafanyia kazi hivyo wanatarajia kuwa kwa kadiri wanavyoendelea kwa kuwa jambo hilo hufanyika kila mwaka watakaokuja Mwaka ujao 2024 wanaamini watafanya vizuri zaidi kwasababu wameona mapungufu na mafanikio yaliyopo kwa wenzao ambao wamewatangulia.

Nao baadhi ya wanafunzi walioshirika katika maonesho hayo Hasani Mbilla pamoja na Cynthia Masuka wanafunzi wa mwaka wa tatu kutoka katika Shahada ya  Sayansi ya Kaya na Taaluma ya Mlaji SUA wamesema katika maonesho hayo wamejaribu kuonesha ni kitu gani ambacho wanakifanya zaidi ili kuwajengea uaminifu na urahisi wa kufanya kazi wakati wa kuelekea Sokoni kwaajili ya kutangaza bidhaa zao na lengo kubwa kutoa mtazamo wa Bunifu kama anasa kwenda kwenye sehemu ya Taaluma.

Wameongeza kwa kukiomba Chuo kuendelea na kile wanachokifanya cha kutoa mafunzo kwa vitendo kwa kuwa kinawafanya wanapotoka nje baada ya kumaliza masomo yao kuwa Imara kwa kujua kitu gani kinahitajika kwenye Soko hivyo wao pamoja na Chuo wanaweza kutangaza vitu ambavyo wanavifanya kwa watu wengine ili kuweza kufika mbali vilevile kuweza kujiajiri na kuajiri wengine.





















Post a Comment

0 Comments