SUAMEDIA

Watunza Kumbukumbu na Makatibu Mahsusi (SUA) wanufaika na Agizo la Rais Samia Suluhu Hassan

 

Na: Tatyana Celestine

Zoezi la utiaji saini makubaliano ya utekelezaji Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) na Vyuo Vikuu na Taasisi wanufaika limeonyesha kuwanufaisha watunza kumbukumbu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kuhudhuria mafunzo yaliyoshirikisha Watunza Kumbukumbu na Makatibu Mahsusi Tanzania ikiwa ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan na kufanya wafanyakazi zaidi ya asilimia 90 kunufaika na mradi huo.

Katika picha ya pamoja washiriki katika mafunzo ya  Watunza Kumbukumbu Tanzania Mjini  Zanzibar 

Akizungumza na SUA Media Mtunza Kumbukumbu kutoka Kampasi ya Katavi SUA, Bi Asha Salum amesema kuwa Mradi wa HEET umekuja wakati muafaka na kuwawezesha wao kujikimu na kulipiwa ada ya mafunzo yaliyofanyika Zanzibar ambapo yamewasaidia kuwajengea uwezo, kuwa wadilifu katika kutunza kumbukubu na siri za serikali pamoja na kujifunza tamaduni za wengine ambao wamekutana kwa pamoja kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Bi Salum ameongeza kuwa SUA kupitia mradi huo kimeona umuhimu kuwawezesha kushiriki kikamilifu hivyo ni wakati sasa wao kutekeleza kwa vitendo yale waliyojifunza, pia chuo kina wajibu wa kutoa ruhusa pale panapohitajika kujiendeleza kielimu ili kuongeza wasomi katika kada hiyo hatimaye kupatiwa idara ili waweze kujisimamia wenyewe tofauti na sasa kuwa chini ya maafisa Tawala.

Kwa upande wake Mtunza Kumbukumbu kutoka Idara ya Rasilimali Watu na Utawala Kampasi ya Edward Moringe Sokoine Bw. Bernald Gereni ameishukuru menejimenti ya SUA kwa kutoa fursa ya kupata mafunzo na kiapo juu ya utunzaji kumbukumbu na utunzaji wa siri, kutekeleza maadili katika kazi zao pamoja na usalama katika eneo la kazi kwani baada ya mwaka mmoja uwajibikaji utaongezeka pamoja na ufanisi kwa kuwa hayo ndio mambo chanya yanayotakiwa katika kila eneo la kazi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mnamo May 27, 2023 alipokuwa akifunga mafunzo ya siku nne katika Mkutano Mkuu wa Mwaka 2023 Mjini Zanzibar aliwataka waajiri kuwaruhusu wafanyakazi wao kushiriki katika mafunzo ya namna hiyo pamoja na kuwapatia fursa ya kuongeza elimu ili kuboresha utendaji kazi na maslahi kutokana na kazi wanazofanya  hivyo kupitia mradi huo tayari SUA imetekeleza kikamilifu.



Katika picha ya pamoja washiriki katika mafunzo ya  Watunza Kumbukumbu Tanzania yaliyofanyika Zanzibar 

 

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments