Na: Amina Hezron,Dodoma
Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na
Biashara imeliomba Bunge kuitengea wizara yake bajeti ya jumla ya shilingi
billion 119 Katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 ili iweze kutekeleza majukumu
yake.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji. |
Maombi hayo yamewasilishwa
bungeni leo jijini Dodoma na Waziri wa
Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.
Ashatu Kijaji wakati akisoma hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha
kwa mwaka 2023/2024.
Amesema katika fedha hizo shilingi
billion 75.4 ni matumizi ya kawaida, ambapo shilingi bil 63 ni mishahara na
shilingi bilioni 12.3 ni matumizi mengineyo.
Ameongeza kuwa shilingi bilioni 43.5
zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambapo shilingi bil 30.3 ni fedha
za ndani na shilingi bilioni 13.2 fedha za nje.
0 Comments