Na: Amina Hezron,Dodoma
Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Viwanda Biashara, Kilimo na Mifugo
imeishauri Serikali kuiongezea uwezo kifedha,rasilimali watu na vitendea
kazi Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili iweze idhibiti bidhaa zisizo na
ubora zinazoingia nchini kwa wingi na kuleta athari kwa watumiaji.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Mhe. Mariamu Ditopile Mzuzuri. |
Hayo yameelezwa leo jijini Dodoma
na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Mhe. Mariamu Ditopile Mzuzuri
alipokuwa akisoma Taarifa ya kamati ya kudumu ya bunge ya Viwanda Biashara
Kilimo na Mifugo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda
na Biashara pamoja na maoni ya kamati kuhusu makadilio ya mapato na matumizi ya
fungu 44 kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Amesema swala la uingizaji wa
bidhaa za chakula nchini limepata sura tofauti kutokana na hali ilivyo duniani
ambapo baadhi ya wafanya biashara wamekosa uaminifu na kutengeneza vyakula
visivyo salama.
“Tumeona kwenye mitandao mchele
usio salama wa plastic ukitengenezwa na kuonekana kama mchele halisi hali hii
inatisha usalama wa wananchi wetu”, alisema Mhe. Mzuzuri.
Hivyo kamati imeomba sekta za
uzalishaji wa bidhaa za viwandani na mazao yatokanayo na kilimo nchini ziwezeshwe
kuzalisha kwa wingi ili kujitosheleza kwa chakula na kupunguza uingizaji wa
bidhaa hizo na kuhakikisha bidhaa zote za chakula zinazoingizwa nchini zina
ubora stahiki kwa usalama wa walaji.
0 Comments