Na: Hadija Zahoro – Morogoro.
Wamilki,wasimamizi
pamoja na walimu wa shule mbalimbali nchini wameshauriwa kujenga tabia ya kuwapeleka wanafunzi kufanya ziara vyuoni kama sehemu ya kuwapa
ufahamu na uwezo wa kuchagua kozi ya kusoma mara baada ya kuhitmu elimu ya
Sekondari.
Picha ya Wanafunzi hao wakiwa kwenye kitengo cha ufugaji wa viumbe maji |
Ushauri
huo umetolewa na Mshauri wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Sega,
Pauline Rusisye, amesema hayo wakati wa ziara ya wanafunzi wa shule hiyo walipotembelea
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ili kujifunza masomo ya sayansi
yanayofundishwa chuoni hapo.
Ameeleza
kuwa wao kama Sega wameamua kuwaleta wanafunzi hao wa michepuo ya Sayansi ili
kuwaonesha fursa zinazopatikana chuoni hapo hivyo, itawajengea wao kuona
uhalisia unaofanyika kulingana na kozi inayosomwa.
‘‘Watoto
wanasema wanataka kuwa madaktari wa mifugo, ili uwe daktari wa mifugo unatakiwa
ufanye nini na wanaosomea kozi hiyo wanafanya vitu gani uhalisia wake upoje na
ndiyo maana wamekuja hapa ili kujifunza mambo ya afya wanyama pamoja na kilimo’’.Anasema
Bi.Rusisye
‘‘Mbali
na hapo wametoka Chuo Kikuu cha
Muhimbili kujifunza Mambo ya afya ya Binadamu,chuo kikuu cha Dar es salaam
kujifunza mambo ya uhandisi na mambo yote yanayohusiana na sayansi hivyo kama
mtoto akimaliza hapo anajua kabisa akimaliza na akaenda SUA au Muhimbili anajua
anaenda kusoma Kozi gani kulingana na Mchepuo anaousomea’’.Anaeleza Bi. Rusisye
Bi.
Rusisye ameeleza kuwa kulingana na dunia ya sasa kubadilika, amewaasa walimu kuweka
mambo wazi kwani mwanafunzi akijionea mwenyewe anapata ujasiri wa kumwelezea mzazi
kitu anachotaka kusomea na kina maana gani hivyo, safari hiyo ni muhimu katika
masomo ya watoto.
Amesema mbali
na hapo wametoka Chuo Kikuu cha Muhimbili kujifunza Mambo ya afya ya
Binadamu,chuo kikuu cha Dar es salaam kujifunza elimu ya uhandisi na yote yanayohusiana na sayansi hivyo kama mtoto
akimaliza hapo anajua akaenda SUA au Muhimbili anajua anaenda kusoma Kozi gani
kulingana na Mchepuo anaousomea.
Kwa
upande wake Mtaalamu wa Maabara ya Sayansi ya Udongo SUA, Mohamed Mohamed ameeleza kuwa kutokana na Wanafunzi
waliofika SUA kujifunza kwa vitendo anatarajia kuwepo kwa ongezeko la Wanafunzi
wakati wa usajili unaofuata kwani
wamepata ufafanuzi mkubwa wa kile kinachofanyika katika maabara hiyo.
Amesema
kuwa kutokana na elimu waliyoipata wanafunzi hao anaamini kuwa wataenda
kuwashauri ndugu, jamii na marafiki zao waje kufanya utafiti wa mashamba yao
pamoja na kusoma kozi ya kilimo inayofundishwa chuoni hapo.
Kwa
upande wao Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Sega, Rebecca James na
Grace Charles wameeleza kuwa mbali na kutazama katika Runinga za Wanyama,
hawakuwahi kushuhudia uhalisia wa namna ya wanavyotibiwa katika hospitali zao
lakini kupitia SUA, wameweza kuona na wanatamani kwenda kusomea kozi hiyo
katika Chuo hicho.
Katika
ziara hiyo ya Wanafunzi hao wa kidato cha nne mchepuo wa Sayansi, wameweza kutembelea
Ndaki ya Kilimo katika Maabara ya Sayansi ya udongo, Hospitali ya Rufaa ya Wanyama,
Kitengo cha Bustani, Idara ya Sayansi ya Wanyama, Viumbe Maji na Malisho pamoja
na Shamba la Malisho katika Shamba la Mfano lilipo Magadu.
BAADHI YA PICHA ZA WANAFUNZI HAO WAKITEMBELEA MAENEO MBALIMBALI YA CHUO.
0 Comments