Na: Gojo Mohamed, Morogoro.
Imeelezwa kuwa takribani vijana
250 wanasafiri kwa mwaka katika nchi mbalimbali duniani kwa shughuli za utarajali
na kujiongezea maaarifa zaidi katika nyanja mbalimbali hususani katika kilimo na mifugo kutoka vyuo vikuu na vyuo vya kati hapa Tanzania.
Vijana hao wanachama wa SUGECO 20 wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mara baada ya zoezi la kuwaaga. |
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa SUGECO bwana Revocatus Kimario wakati wa halfa fupi wakiwaaga vijana 20 wanaosafiri kuelekea nchini Denmark kwa ajili ya shughuli za utarajali yaani internship kwa muda wa miezi 12-18
iliyofanyika katika Ushirika wa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUGECO.
Kimario amesema SUGECO wanayo
furaha kubwa kwa sababu walikuwa wa kwanza kuanzisha program za internship kwa
kuwapeleka vijana nchini Izrael hasa katika sekta ya Kilimo na Mifugo lakini kwa
sasa program hii imekuwa kubwa na wanapeeka vijana zaidi ya 250.
Mkurugenzi huyo amesema mwaka 2018 SUGECO
imesaidia vijana wengi Kwenda nchini Marekani na kufikia sasa kuna vijana 422
ambao wamenufaika katika mafunzo hayo ya intership.
Naye Bwana Steven Michael ambaye ni Mkurugenzi wa masoko na uzalishaji kutoka wizara ya mifugo na uvuvi ameipongeza SUGECO kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita hasa katika sekta ya mifugo na uvuvi.
Amesema kuwa kutokana na mchango
wa SUGECO katika sekta ya Mifugo ya Uvuvi, Wizara hiyo itaendelea kushirikiana
nao katika kuandaa mpango mkakati baada ya intership vijana wanaporudi nchini uwasaidie kuweza kutumia maarifa
waliyoyapata nchini Denmark kuchangia Sekta ya Mifugo na Uvuvi kupitia vituo
atamizi vilivyoanzishwa na Wizara.
Kwa Upande wao Bi. Veronica
aloyce na Bw. Fahadi Mwijuma ambao ni
baadhi ya vijana wanaotarajia kusafiri Kwenda nchini Denmark wiki hii
wamesema kuwa wanamatarajio makubwa ya
Kwenda kujifunza na mara watakaporudi nchini wataendeleza maarifa na ujuzi walioupata kwa kujiajiri kwa kuanzisha
mashamba yao binafsi na kuweza
kuwasaidia vijina wenzao katika maswala ya mifugo.
Hata hivyo SIGECO kwa
kushirikiana na taasisi ya fedha ambayo ni Benki ya EQUITY imeweza kutoa mikopo
kwa vijana hao wanaonufaika na hizi program tangu zilipoanzishwa mwaka 2018.
Aidha kwa usimamizi ambao SUGECO
imetoa kwa vijana hao kuhakikisha mikopo hii inarejeshwa hivyobenki hiyo
kuendelea kujenga imani na SUGECO ambapo pia imeweza kutoa fedha kwa ajili ya
kutekeleza program ya Kizimba inayoratibiwa na SUGECO ambayo itatengeneza fursa
za ajira kwa vijana kupitia minyororo ya thamani ya kilimo biashara.
Mkurugenzi mtendaji wa SUGECO bwana Revocatus Kimario akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo. |
Bwana Steven Michael ambaye ni Mkurugenzi wa masoko na uzalishaji kutoka wizara ya mifugo na uvuvi akikabidhi nyaraka za safari kwa mmoja wa vijana nao.. |
0 Comments