Na:
Gerald Lwomile, Dodoma
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo
Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)
Prof. Maulid Mwatawala ametoa rai kwa wabunifu wa Vyuo Vikuu nchini wakiwemo wa
SUA kuhakikisha wanakuwa na ubunifu wenye viwango vya juu.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam SUA Prof. Maulid Mwatawala akisisitiza jambo wakati akiongea na wabunifu kutoka SUA hawapo pichani (Picha zote na Gerald Lwomile) |
Prof. Mwatawala ametoa rai hiyo Aprili 28, 2023 wakati akizungumza na wabunifu kutoa SUA kwenye maonesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Amesema kuwa ubunifu uko katika
ngazi mbalimbali kuanzia kwa wananchi wa kawaida, Vyuo vya Kati
na Vyuo vya Juu, hivyo matarajio ya wananchi wengi ni kupata matokeo mazuri
zaidi ya bunifu kutoka vyuo vya juu.
“Sisi tunatakiwa kwenda kiwango
cha juu zaidi cha ubunifu, kwa mfano mtu anabuni kitambaa cha nguo ahakikishe
mchanganyiko wa malighafi kama pamba na siliki katika nguo hiyo unaweza
kumsaidia mtu kujua kitambaa cha nguo hiyo kinaweza kuvaliwa wakati gani”
amesema Prof. Mwatawala
Wakati huo huo Mbunge wa Iringa
Mjini Mhe. Jesca Msambatavangu aliyepata muda wa kutembelea banda la SUA
amewapongeza watafiti katika chuo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Jesca Msambatavangu (aliyevaa kombati katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wabunifu kutoka SUA |
Amesema matunda ya tafiti
mbalimbali zinazofanywa katika chuo hicho yameendelea kuonekana katika maeneo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na mkoani Iringa ambako tafiti kadhaa zimefanyika.
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
kimefanya tafiti mbalimbali Mkoani Iringa ikiwemo utafiti wa kudhibiti mlipuko
wa panya ambao walikuwa wakileta hasara ya asilimia 100 kwa kula mazao ya
wakulima katika maeneo mbalimbali kama Uyole, Mkungugu, Isimani na Izazi.
Msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba (mwenye rasta) akisikiliza maelezo ya ubunifu |
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nelson Mandela upande wa Utawala, Fedha na Mipango Prof. Suzan Augustino kulia akifurahia bunifu mbalimbali za SUA |
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam SUA (kushoto) akimsikiliza mbunifu kutoka SUA |
Bi.Theresia Temu kutoka SUA akiwa amembeba panya anayeweza kutambua eneo ambalo limetegwa bomu au makohozi yenye vimelea vya Kifua Kikuu |
0 Comments