SUAMEDIA

SUA kutengeneza chanjo ya magonjwa ya Samaki

 

Na Gladness Mphuru

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kipo kwenye mkakati wa kutengeneza chanjo za papo kwa papo (Autovaccine) dhidi ya magonjwa ya Samaki ambayo yanaathiri afya ya binadamu.


Prof. Robinson Mdegela akitoa maelezo ya namna wanavyofanya jitihada kutengeneza chanjo ya magonjwa ya Samaki

Hayo yamebainishwa Februari 7, 2023 na Mhadhiri Mwandamizi kutoka Ndaki ya Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya SUA Prof. Robinson Mdegela, wakati akifanya mahojiano na vyombo vya habari kwenye Kituo cha Utafiti cha Magonjwa ya Samaki Kampasi Kuu ya Edward Moringe Mkoani Morogoro.

Hapa kwetu tunachokifanya, tunapita kwenye mashamba ya wafugaji, vituo vya uzalishaji, tunatumia njia za kitaalamu kupata hao bakteria na kuja nao maabara kutengeneza mbegu ya hiyo chanjo kisha tunaitunza maabara, ikitokea ugonjwa huo umelipuka tunachukua mbegu hiyo tunamsaidia mkulima kuchanja mifugo yake" amesema Prof. Mdegela

Amesema kuwa yapo magonjwa ya Samaki ambayo haya muathiri binadamu kama vile Ndui inayotokana na Virusi, pia yapo magonjwa ya Samaki yanayomuathiri binadamu lakini wanaendelea na tafiti ili kupata suluhu ya magonjwa yanayosababishwa na kimelea aina ya bakteria.

Ameongeza kuwa wanyama hasa Samaki wanaoishi miaka mingi wanauwezekano pia wa kupata ugonjwa wa Kifua Kikuu, lakini changamoto hiyo haipo kwa Samaki wanaofugwa kwa muda wa miezi 6 hadi 8.

Hii inawapata Samaki wenye umri mkubwa ambao hufugwa kwa ajili ya mapambo bahati nzuri tunatoa hiyo elimu na tuna wataalamu wetu ambao kwa sasa wanawafikia wafugaji huko walipo, wanachukua sampuli za maji  udongo, mazingira, Samaki wenyewe, kwa wavuvi na kwenye nyavu zao na ili kugundua kama kuna changamoto ya afya inayotakiwa kutatuliwa" amesema Prof. Mdegela

Post a Comment

0 Comments