Na; Winfrida
Nicolaus
Katika
kuhakikisha ushirikiano baina Tanzania na Ufaransa unaimarika Balozi wa
Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil
Hajlaoui amefanya ziara katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha
Kilimo (SUA) ili kujua maeneo ya kimkakati ambayo Ufaransa inaweza kushirikiana
na Chuo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda (kulia) akimkaribisha Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui (Picha zote na Gerald Lwomile)
Hayo yamebainishwa Februari 6, 2023 mkoani Morogoro na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Esron Karimuribo, wakati wa ziara ya Balozi huyo katika Chuo Kikuu cha Sokoine.
Amesema
ujio wa Balozi huyo wa Ufaransa SUA ni wa baraka kwani umekuwa na matokeo
mazuri zaidi katika kusikiliza mawazo ya kibiashara kutoka kwa vikundi na makampuni
ya wanafunzi chuoni hapo ambapo amewahakikishia kuwaunga mkono na kuahidi
kuwatafutia soko kutokana na bidhaa wanazozalisha.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui (katikati) akiendesha majadiliano katika ukumbi wa Baraza wa SUA, (kushoto) ni Prof. Karimuribo
Prof.
Karimuribo amesema matokeo mengine ni kwamba kwa wale ambao wametoa mawazo
mazuri kupitia Mradi wa ’Innoversity’ Balozi ameyapenda hivyo ameyapa baraka na
wanategemea kuwa hatua inayofuata ni kuyachanganua ili wapate wanafunzi ambao
wataenda nchini Ufaransa kati ya mwezi wa Nne na wa Sita, 2023 kwa ajili ya
kujifunza ili watakaporudi waweze kuendeleza mawazo yao kibiashara.
“Kuna
kundi la wale ambao wanatengeneza au kufanya Samaki kama mapambo majumbani hata
maofisini Balozi amesema yuko tayari kuhakikisha anayaunga mkono na jambo zuri
ni kuwa tumebahatika tu kwamba kupitia Programu ya STEPS ya SUA ambayo inawasaidia
na kuwahamasisha wanafunzi wajiunge halafu wasajili Makampuni yao ya kibiashara
wakati wakiendelea na masomo sasa kupitia uhamilishaji huo kumechangia kwa
kiasi kikubwa hata kupata mawazo mazuri”, amesema Prof Karimuribo
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui (wa pili kushoto) akikagua moja ya majengo yaliyoko SUA, (mbele aliyevaa Kaunda Suti) ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Maulid Mwatawala
Amesema
wapo wengine ambao wanatengeneza Unga wa Mchicha (AMARATH) wenye Madini ya
kutosha, Vitamini ya kutosha kwa ajili ya kuwasaidia kinamama wajawazito pamoja
na watoto wenye Utapiamlo hawa nao wazo lao litaboreshwa Zaidi.
Prof.
Karimuribo ameongeza kuwa SUA ni Taasisi ambayo inatoa Taaluma lakini kwao kama
Chuo wanaona ni matokeo mazuri kwa kuwa kupitia ushirikianao huo wale wanafunzi
ambao wanawafundisha wanatoka chuoni hapo wakiwa tayari ni wajasiliamali na
wana makampuni yao hivyo hawatategemea kuajiriwa nao kutoa fursa za ajira kwa
wengine.
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania HE Nabil Hajlaoui (kulia) akiangalia matunda aina ya Zabibu yanayolimwa kwa majaribio katika Shamba na Mafunzo la SUA mkoani Morogoro, (kushoto picha ya juu) Mkuu wa Idara ya Shamba la Mafunzo SUA Dkt. Newton Kilasi (Picha na Gerald Lwomile)
0 Comments