Na: Calvin Gwabara - Katavi.
Wanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda wameushukuru Uongozi wa Chuo kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) kwa kuwajengea uwezo wa kufahamu na namna ya kuingiza masuala ya Jinsia katika shughuli mbalimbali za Chuo.
Kiongozi wa Masuala ya Jinsia kwenye Mradi wa (HEET) Prof. John Jeckoniah akieleza lengo na mafunzo hayo.
Akifungua mafunzo hayo Januari
9. 2023 Rasi wa Ndaki ya Mizengo Pinda Prof. Josiah Katani amesema mafunzo hayo
yamekuja wakati muafaka kwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi kimazoea kwa
kuchukulia maswala ya jinsia kama swala la kawaida lakini kumbe ni jambo ambalo
linawagusa katika kazi zao za kila siku.
“Mafunzo ya aina hii huwa
hayapatikani kirahisi kama ambayo tumepata leo ni kwa siku moja lakini
yamefungua uelewa wa watu wengi kuhusu maana na masuala mazima ya Jinsia na
namna ya kuyatumia katika kazi zetu za kila siku na tunaomba mafunzo ya aina
hii yaendelee maana kadri watu wanavyozidi kujengewa uwezo ndivyo wanavyozidi
kudadisi na kuona njia bora za kutumia jinsia kwenye kazi zao za kila siku”
alisema Prof. Katani.
Aidha Prof. Katani amependekeza
maswala ya Jinsia kuangaliwa namna ya kuingizwa kwenye programu na kozi
zinazotolewa na SUA na kuweza kufundishwa kama mada kwa wanafunzi wa kozi zote
bila kujali wanasomea Misitu, Kilimo, Udaktari na zinginezo zote zinazotolewa
SUA.
Aidha ameushukuru Mradi wa HEET
na Wataalamu wa Jinsia waliofika kutoa mafunzo hayo na wanaamini mradi huo
utaleta mafanikio makubwa katika utekelezaji wake ili kuleta mafanikio zaidi
kwa chuo.
1. Rasi wa Ndaki ya Mizengo Pinda Prof. Josiah Katani akitoa shukrani zake na neno la ufunguzi wa mafunzo hayo.
Akieleza lengo la mafunzo hayo
Kiongozi wa Masuala ya Jinsia kwenye Mradi wa
(HEET) Prof. John Jeckoniah amesema ni kuwajengea uwezo Wanataaluma,
Waendeshaji na Wanafunzi kufahamu na
kuingiza maswala ya Jinsia katika shughuli zote muhimu za utendaji wa chuo
jambo ambalo ni kwa mujibu wa miongozo ya chuo na Taifa.
“Mafunzo haya ni muhimu sana
maana yanawajengea uwezo Wanataaluma na Wanafunzi kutambua masuala ya Ukatili
na unyanyasaji wa kijinsia ambayo yanaweza kuwatokea katika mazingira yao ya
kazi au ya masomo na jinsia ya kuchukua hatua au kutoa taarifa ili watu
waliopewa dhamana ya kuyashughulikia waweze kuchukua hatua” alieleza Prof.
Jeckoniah.
Kiongozi huyo wa masuala ya
Jinsia amesema SUA ina Sera ya Jinsia, Rasimu ya sera ya kupinga unyanyasaji na
ukatili wa kijinsia ambayo itakamilika hivi karibuni hivyo mafunzo hayo ni
sehemu ya kuwaandaa wadau hao muhimu katika utekelezaji wa uundwaji wa Dawati
la Jinsia kwa mujibu wa maagizo ya Serikali ambayo yameelekeza vyuo vyote vya
Elimu ya Kati na Juu kuwa na Dawati la Jinsia.
Prof. Jeckonia amefafanua
Dawati la Jinsia ni mfumo rasmi ambao unawezesha Wafanyakazi, Wanafunzi na
Wadau wengine wote wanaofanya kazi na chuo kuweza kutambua masuala ya kijinsia
na namna ya kuyashughulikia na kwamba miongozo hiyo inakifanya Chuo kutekeleza
shughuli zake kwa kuzingatia malengo mahususi kama ya chuo.
Kwa upande wake Makamu Rasi wa Ndaki ya Mizengo Pinda upande wa Taaluma Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Prof. Anna Sikira amesema mafunzo hayo yatawasaidia sana namna ya kutengenza mazingira bora ya kusihi na kushirikiana kati ya Wafanyakazi, Wadau na Wanafunzi hasa ikizingatiwa kuwa wengi wa wanaokuja kusoma hapo ni bado ni watoto wadogo wanahitaji malezi na uangalizi ili kuweza kufikia malengo yao.
“Wanafunzi wetu wengine ni wadogo sana na walipokuwa nyumbani na shule za Sekondari walikuwa na maisha ya kufungiwa na kulindwa sana lakinI wanapofika chuoni wanakuwa huru tukiamini ni watu wazima wenye zaidi ya miaka 18 hivyo wanahitaji bado uangalizi na elimu ya namna ya kuishi katika uhuru walionao kwa kufuata miongozo, sheria na kanuni za chuo kwa hiyo mafunzo haya ni muhimu sana kwao na walimu wetu” alifafanua Prof. Sikira.
Amesema Dawati la Jinsia
litasaidia kupokea masuala yote yanayohusu Jinsia maana sasa Wanajumuiya
watakuwa wanajua sehemu husika ya kupeleka mambo hayo maana kwa upande wa
Wanafunzi wanapeleka kwa mshauri wa wanafunzi na wengine hawapeleki kutokana na
mazingira lakini dawati litakuwa sehemu salama na muhimu wa kushughulikia
masuala hayo Chuoni.
1.
0 Comments