SUAMEDIA

SUGECO kueendelea kupeleka wahitimu na wanafunzi wa SUA nje ya nchi

Na Gojo Mohamed

Ushirika wa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUGECO) umeendelea kuwapatia vijana fursa kwa kuwapeleka nchi mbalimbali Duniani ikiwemo Denmark, kwa ajili ya mafunzo ya utarajali ili kuwaongezea ujuzi na maarifa katika sekta ya Mifugo.


Dkt. Othaman Mohamed  akimkabidhi cheti na tiketi ya Ndege Bi. Phinna Ngowi anayeelekea nchini Denmark kwa ajili ya mafunzo

Hayo yamebainika katika hafla fupi iliyofanyika Januari 9, 2023 Makao Makuu ya Ushirika huo Mkoani Morogoro ambayo imehudhuriwa na Uongozi wa SUGECO pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa ajili ya kuwaaaga baadhi ya vijana wanaotarajia kwenda nchini Denmark hivi karibuni.

Kwa upande wake Dkt. Othaman Mohamed kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, ameipongeza SUGECO na kuongeza kuwa Wizara hiyo inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Ushirika huo, kwani vijana hao watakaporudi nchini mara baaada ya mafunzo wataleta chachu ya maendeleo na mabadiliko katika sekta ya Mifugo nchini.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya SUGECO Dkt. Anna Temu amesema kuwa zoezi hilo lilianza kwa kuwapeleka vijana kupata ujuzi nchini Israeli na Marekani lakini kwa sasa wanawapeleka vijana katika nchi ya Denmark na wataendelea kuwapeleka katika nchi zingine, na ameongeza kwa kuwakaribisha vijana SUGECO ili kupata ujuzi hasa katika maswala ya kilimo pamoja na mifugo.


Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kutoka Usharika wa SUGECO wakiwa katika hafla fupi ya kuagwa 

Kwa upande wake Ibrahimu Hassan ambae ni miongoni mwa vijana wanaotarajia kwenda nchini Dermak kwa ajili ya mafunzo ya utarajali, amesema kuwa matarajio yake ni kupata ujuzi kwa ufanisi zaidi ili kuwasaidia vijana wenzake kutokana na ujuzi huo, pia ameshukuru kwa kupata fursa hiyo  na kuupongeza uongozi wa SUGECO  kuhusani katika  program.

Mafunzo hayo ya utarajali yatakuwa kwa muda wa miezi kumi na nane 18 kwa vijana kujifunza na kupata ujuzi katika sekta Ufugaji na wanatarajia kupeleka vijana 56 nchini Denmark kwa mwaka huu.



Post a Comment

0 Comments