SUAMEDIA

Wananchi wa Nabinda waoanja matunda ya Uhifadhi wa Misitu ya Vijiji.

 Na; Calvin Gwabara,  Lindi

Wananchi wa Kijiji cha Nambinda Kata ya Mlembwe Wilayani Masasi Mkoani Lindi wafanikisha kuanza ujenzi wa Zahanati ya Kijiji ili kuokoa maisha ya Wananchi kutokana na fedha zitokananzo na faida za utunzaji misitu kwenye Kijiji chao kupitia Mradi wa kuhifadhi misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya mazao ya misitu Tanzania (CoForEST).


Jengo la zahanati likiwa katika hatua za ujenzi

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho bwana Said Abdallah Kowe wakati akiongea na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari na viongozi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) wanaotekeleza mradi huo kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC).

Sisi kama wanakijiji cha Nambinda kabla haujafika huu mradi Kijijini tulikuwa tunatamani kupata zahanati lakini ilikuwa imeshindikana kwa sababu kutoka Nambinda hadi Kijiji cha Mlembwe ambako tunapatia huduma za afya ni umbali wa Kilometa 8 ambapo wakinamama wamekuwa wakijifungulia njiani na Watoto kufariki lakini pia wagonjwa wengine wenye hali mbaya kukosa matibabu karibu na hivyo kufia njiani lakini sasa baada ya kuja mradi huu tumekubaliana fedha zote tunazozipata kutokana na rasilimali mistu tunajenga jingo la Zahanati” alieleza Bwana Kowe.

Aidha Mwenyekiti huyo wa Kijiji amebainisha kuwa toka wameanza ujenzi huo wameshatumia Zaidi ya shilingi milioni 33,400,000 na tayari wamepitisha tena Zaidi ya shilingi milioni tatu kwaajili ya kununua Saruji ya kumalizia boma na mhandisi wa ujenzi amewashauri kuongeza jingo kwaajili ya Wazazi na hivyo kuiomba Serikali kuu pia kuwaongezea nguvu kutokana na hatua mbayo tarai Kijiji kimefika.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho bwana Said Abdallah Kowe wakati akiongea na Waandishi wa Habari.

Amebainisha kuwa jingo zima la zahanati hiyo hadi kukamilika kwake limekadiriwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 125 na hadi sasa wameshatumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 36 na bado wanaendelea na ujenzi kupitia makusanyo ya fedha kutokana na rasiliamali misitu ambayo wanaitunza na kuilinda hasa mbao.

Kwa upande wake Mzee Hemed Kipaga Mkazi wa Kijiji hicho amesema kumekuwa na mafanikio makubwa katika Kijiji chao tangu kuanza kwa mradi huo ambao umewapitisha kwenye mafunzo mbalimbali ya utawala bora, Uchomaji Mkaa, Jinsi na Jinsia na mengine mengi ambayo yamesaidia kuongea uelewa kwenye shughuli za usimamizi wa misitu ya jamii na manufaa ya misitu yao.

Amesema pamoja na kuanza kwa mpango wa uvunaji lakini msitu wao umeimarika zaidi maana hauingiliwi na chochote hasa majangili ambao walikuwa wakiingia kabla ya mradi na kuchoma mkaa na kuvuna mbao bila utaalamu na pia kuchoma moto na kukosesha Kijiji mapato.

” Mimi naona elimu ya Utawala bora imesaidia sana hasa kwenye usimamizi wa misitu yetu miwili ya Kijiji lakini pia ndio sababu tunaona sasa hata fedha zinatumika vizuri Kijiji chetu kinajenga zahanati nzuri na ya kisasa kwhiyo tunawashukuru TFCG na MJUMITA kwa elimu hii na kutuletea mradi huu ambao ni chachu ya maendeleo kwenye Kijiji chetu.” alieleza Mzee Kipaga.

Akizungumzia mabadiliko anayoyaona kwenye elimu ya Jinsi an Jinsia iliyotolewa na mradi Bi. Yanini Makanga ambaye ni Mhasibu wa kamati ya maliasili ya Kijiji hicho cha Nambinda amesema kuwa mgawanyo wa majukumu kwenye familia umeimarika kwani huko nyuma kazi za mwananke anafanya mwanamke na kazi za mwanaume anafanya chache na zingine kuzicha kwa mwanamke nah ii kuwapa mzigo mkubwa wanawake kwenye kaya.

”Baada ya Kwenda kwenye mafunzo tuliporudi tulitoa elimu kwa wananchi wengne kijijini na pia kwa waume na wake zetu na kweli tunaona mabadiliko maana mfano mume wangu ananisaidia kazi mbalimbali ambazo awali alikuwa hafanyi mfano kumhudumia mtoto n ahata kukata kuni na kupika muda mwingine anapika kwahiyo upendo naona umeongezeka.

Mradi wa CoForEST unatekelezwa katika vijiji 41 vilivyopo kwenye wilaya za Morogoro, Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro, Liwale, Ruangwa na Nachingwea mkoani Lindi na Kilolo mkoani Iringa.

Post a Comment

0 Comments