SUAMEDIA

Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Misitu, Wanyapori na Utalii SUA washiriki zoezi la usafi chuoni

 

Na Gojo Mohamed - Morogoro

Katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa viumbe hai pamoja na jamii, wanafunzi wanaosoma Shahada kutoka Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameaswa kushiriki katika zoezi la  kufanya usafi kwani jambo hilo ni la msingi na endelevu litawasaidia katika masomo yao  pia kwa Afya ya Jamii kwa ujumla.

Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii SUA wakiwa katika zoezi la usafi

Hayo yamezungumzwa na Mhadhiri Msadizi kutoka Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Bw. Japhet Mwambusi  ambaye alimwakilisha Kaimu Rasi wa Ndaki hiyo, Dkt. Agnes Sirima katika zoezi la  usafi, kupewa mafunzo ya ufugaji wa nyuki na uongezaji thamani wa mazao ya nyuki vilevile faida za upandaji miti ambalo lilifanyika katika Bustani ya Mimea yaani  Botanic Gadern katika Kampasi ya Edward Moringe iliyopo chuoni hapo .

Bw. Mwambusi Amesema wanafunzi wakiwa masomoni washirikiane na jamii pamoja na wadau mbalimbali katika kuhifadhi mazingira  ili  kuzidi kuonesha mchango wao katika shughuli hizo jambo litakalowapatia uzoefu utakao wasaidia mbeleni.

Mhadhiri Msadizi kutoka Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Bw. Japhet Mwambusi akizungumza na wanafunzi hawapo pichani

Aidha Bw. Mwambusi ameongeza kuwa mafunzo hayo waliyopata yanaweza kuwasaidia wanafunzi katika masomo lakini pia mara baada ya kuhitimu  watapata fursa ya kuanzisha makampuni yao binafsi  kama vile ya uzalishaji wa miti na asali wanachotakiwa kufanya ni kuendelea kuzingatia masomo kama haya yatolewayo SUA .

Naye Mwenyekiti wa Tanzania Forest Students Association (TFSA) Msumi Mkomwa ameshukuru na kusema kuwa katika zoezi hilo wemeweza kupata elimu juu ya ufugaji wa nyuki na mazao yake uongezaji thamani ya mazao yatokanayo na misitu pamoja na  kufanya utalii wa ndege .

Kwa upande wake mmoja ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza Bw. Asililo Bujimu amewashauri wanafunzi wenzake kutosita kwenda kushiriki katika usafi wa mazingira ili waweze kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitawasaidia katika masomo pamoja na maisha yao mara baaada ya kuhitimu  elimu ya Chuo .

Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Misitu kutoka Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii SUA wakiwa katika matukio tofauti siku ya zoezi la usafi








Post a Comment

0 Comments