Na : Gojo Mohamed.
Uniti
takribani 50 za damu zimefanikiwa kukusanywa kutoka kwa Wanafunzi
pamoja na wanajumuiya wa Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) katika
zoezi la uchangiaji wa damu zitakazoenda kuwasaidia wagonjwa katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Wanajumuiya ya SUA wakichangia damu katika bonanza hilo |
Amesema
hayo Afisa Mhamasishaji Uchangiaji wa Damu kutoka hospitali hiyo,Bw. Mabruk
Mbaruku kuwa katika Zoezi la uchangiaji
damu lililoambatana na Bonanza la michezo mbalimbali kwa pamoja yamefanyika katika Viwanja vya Kampasi Kuu vya Edward Moringe Sokoine.
Bw.
Mbaruku ameeleza kuwa zoezi la uchangiaji wa damu ni muhimu sana kwa sababu
hakuna sehemu ambayo unaweza ukapata damu zaidi ya kwa binaadamu mwenzio
kwahiyo ni lazima jamii ihamasike ili iweze kuchangia damu.
Kwa
upande wake SUA Dkt Charles Lymo kutoka Idara ya Sayansi ya Wanyama Viumbe Maji
na Nyanda za Malisho, amesema kuwa wanajamii
wanapaswa kujijengea tabia ya kuchangia damu kwa sababu suala la ukosefu wa damu ni la dharula ili kuhakikisha
vituo vinavyotunza damu vinakuwa na damu
ya kutosha kwa ajili ya kuokoa maisha yao
na ya watu wengine.
‘‘Suala la uchangiaji wa damu ni
muhimu, tunasikia kunakuwa na takwimu za ajali, lakina Wamama wanajifungua na
wanakosa damu na kupelekea kupoteza maisha yao kwa hiyo benki zetu za damu
zinapokuwa na damu ya kutosha inapelekea kuokoa Maisha ya watu na vizuri kuwa
na utaratibu wa kuchangia damu kwa
sababu inakuwekea akiba na wewe mwenyewe pindi upatapo changamoto ya upungufu
wa damu’’. alisema Dkt. Lymo.
Nae,
Fatma Ibrahimu ambaye ni Mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Wanyama
amesema kuwa ameweza kujitokeza katika zoezi la uchangiaji wa damu kwa mara yake
ya kwanza kutokana na umuhimu ambao ameuona ambapo kuna wagonjwa wengi
wanahitaji damu na zinakuwa zinakosekana.
Pia,amesema
kuwashauri wanafunzi wenzie kujitokeza katika kushiriki masuala ya kijamii
ikiwemo hilo la uchangiaji wa damu.
MATUKIO KATIKA PICHA YA BONANZA HILO LILILOKWENDA SAMBAMBA NA ZOEZI LA UCHANGIAJI WA DAMU.
0 Comments