SUAMEDIA

Magonjwa yatajwa kukwamisha ukuaji wa sekta ya Mifugo Mchini.

 Na: Adam Maruma - Dodoma.

Imeelezwa kuwa uwepo wa   magonjwa mbalimbali yayoshambulia mifugo nchini ndio sababu ya kutokuendelea kwa sekta hivyo  na hivyo kuwa na mchango mdogo kwa wafugaji na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa akitoa tuzo kwa Mmoja wa wadau wa kampuni zilizowezesha Mkutano huo.



Hayo yamesemwa na mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akifunga kongamano la kisayansi na  mkutano mkuu  wa 40  wa  mwaka wa Chama cha madaktari wa wanyama  Tanzania  TVA, katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

Mkuu huyo wa mkoa amesema sekta ya Mifugo na Uvuvi ni   muhimu katika kuihakikishia nchi usalama wa Chakula haswa Protini, hivyo  magonjwa mengine  husababishwa na kitendo cha wafugaji kuhamahama na kusambaza magonjwa  hivyo amewataka  watalaam wa mifugo kuja na suluhiho la tatizo hilo.

Ameongeza kuwa changamoto nyingine kubwa ni kwa wafugaji kutotaka kubadilika na kuendana na wakati uliopo kwa kupunguza idadi ya mifugo yao na kubaki na  mifugo michache  na kafugwa kisasa jambo ambalo linahitaji elimu kutoka kwa wataalamu hao wa TVA ili kuongeza tija.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akifunga kongamano la kisayansi na  mkutano mkuu  wa 40  wa  mwaka wa TVA.


‘’Bado kumekuwa na mwitikio mgumu sana ambao tunasumbuana wa wafugaji juu ya kubadilika kutoka kufuga mifugo ya mingi na kuonekana na kwenda kwenye mifugo ya kisasa na bora haswa kwa ngombe,kwenye kuku angalau kumeenda haraka huku hamna shida watu wanaona faida kwenye kuku ni ya haraka kuliko ngombe,’’alieleza Mhe. Rosemary.

Mkuu huyo wa wa mkoa wa Dodoma amewataka madaktari walio kwenye  maeneo mbali nchini kutimiza wajibu wao wa kitaaluma na kiutendaji ikiwepo kuripoti milipuko wa ugonjwa yoyote katika maeneo yao kwa kufuata utaratibu, sheri na miongozo ya Serikali huku akiwataka viongozi kuwachukulia  hatua za kinidhamu wataalam  wachache wanaochafua fani hiyo ili Wananchi waweze kuwaamini.

Kwa upande wake mweneyekiti wa Chama cha Madaktari wa Wanyama Tanzania TVA, Prof. Ezron Karimuribo amesema Chama hicho  kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya  uhaba wa madakatari wa mifugo hasa katika ngazi ya mkoa na wilaya na kusema tatizo hilo linakwenda kinyume na sheria ya magonjwa ya wanyama ya mwaka 2003 inayoelekeza kila Wilaya au Mkoa kuwa na angalau Daktari ya Wanyama mmoja.

‘’Mheshimiwa mgeni rasmi kumekuwa na changamoto ya uhaba wa madaktari wa mifugo katika ngazi ya wilaya au mkoa hivyo kwenda kinyume na sheria yetu ya magonjwa ya wanyama ya mwaka 2003, ambayo pamoja na mambo mengine inaelekeza kila Wilaya au Mkoa kuwa na angalau na Daktari wa wanyama mmoja,kwa ajili ya kukamilisha mahitaji ya kisheria,na  tatizo hilo limesabishwa na kukosekana kwa ajira ya Serikali kwa muda mrefu’’  alisema Prof. Karimuribo.

Aidha ametaja changamoto nyingine katika sekta ya mifugo kuwa ni pamoja na uwepo wa magonjwa mengi ya mifugo ambayo husabishwa na uhaba wa madakatari wa mifugo katika maeneo mbalimbali ya nchi,na hivyo kundelea kwa mlipuko wa magonjwa ambayo si  tu inaleta athari kwa mfugaji bali hata taifa kwa ujumla kwa kuwa taifa linapoteza mapato mengi katika sekta ya mifugo kwa kukosa kupeleka nyama, maziwa na ngozi nje ya nchi na kukosesha taifa fedha za kigeni.

Aidha Mwenyekiti huyo alimweleza pia mgeni rasmi Kile alichokiita Ombwe la muda mrefu  kati ya  ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara mama ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kutoteua angalau Daktari wa mifugo ambaye atakuwa kiungo  kwenye jukumu la kushauri na kusimamia utekelezaji  wa sera inayohusu masuala ya madaktari wa wanyama Tanzania na hivyo kumoumba mgeni rasmi kulifikisha ombi katika wizara husika kwa sababu kwa sekta ya afya imewezekana.










Post a Comment

0 Comments