SUAMEDIA

Watu milioni 20 hufariki dunia kwa mwaka kutokana na shambulio la Moyo

Na Editha Mloli

Vifo vingi vianyotokea duniani asilimia kubwa hutokana na ugonjwa wa Shambulio la moyo, ambapo takwimu zinaonyesha watu milioni 20 hufariki dunia kwa mwaka kutokana na na ugonjwa huu, huku ikielezwa kuwa kila baada ya sekunde 40 mtu hupata shambulio la moyo au kufariki dunia.

PICHA NA MTANDAO


Hayo yameelezwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na kiongozi wa hospitali za SUA Dkt. Omary Abdalah Kasuwi wakati akizungumza kuhusiana na ugonjwa wa shambulio la moyo na kuongeza kuwa ugonjwa huu ni hatari  na unaongoza kwa kusababisha vifo kwa wanaume na wanawake kwenye nchi nyingi duniani.

Ameeleza kuwa shambulio la moyo hutokea pindi tu mtiririko wa damu kuelekea kwenye misuli ya moyo unapokatishwa na Ikiwa mtiririko wa damu haukurejeshwa haraka misuli ya moyo inaweza kuharibika na kusababisha kifo kutokana na ukosefu wa hewa ya oksijeni.

Dkt. Kasuwi ameeleza kuwa  Shambulio la moyo husababisha maumivu makali au ya kadri katikati ya kifua na yanaweza kurejea tena baada ya kitambo kidogo, Kujisikia vibaya maumivu ya mkono mmoja au mikono yote, Kichefuchefu, kutapikakizunguzungu na jasho.

Amesema mtu akipata shambulio la moyo na mtu aliye karibu yake kumuanzishia huduma ya kwanza pamoja na kumpeleka kituo cha Afya na kuanzishiwa matibabu ndani ya saa 1 baada ya kuanza kwa dalili za ugonjwa huo kuna uwezekano mkubwa wa kuokoa Maisha yake na hata kuzuia ulemavu wa kudumu.

“Kama kutakuwa na damu iliyoganda hilo donge la damu iliyoganda kama litaendelea kuku ana kuwa kubwa sana, litaziba kabisa ateri na kuzuia mtiririsho wa damu yenye oksijeni kufika kwenye misuli ya moyo na hivyo kusababisha shambulio la moyo ambapo kama mgonjwa asipopata matibabu kwa wakati kuna hatari ya kumpoteza”. Amesisitiza Dkt. Kasuwi.

Daktari bingwa huyo ameitaka jamii kuwa na utamaduni wa kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya pindi wanapohisi maumivu wasiyoyaelewa ili kupima na kupata ushauri wa kitalam, lakini pia kubadili mtindo wa Maisha ambao kwa sasa unasababisha magonjwa mengi na kupelekea vifo vya watu wengi. 

 




Post a Comment

0 Comments