Na: Calvin Gwabara - Morogoro.
Wadau wa Misitu nchini wametakiwa kushirikiana
na kuisaidia Serikali kuona uwezekano wa Mkaa unazozalishwa kwenye maeneo
mbalimbali nchini kuanza kuuzwa kwa kilo kama badala ya magunia ambayo
yanachangia kutokuwepo kwa usawa katika biashara hiyo na kuharibu misitu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi
Msaidizi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) bwana Emmanuel
Lyimo wakati akizungumza na kutoa mchango wake kwenye mkutano wa Wadau wa Kikosi
kazi cha Misitu Tanzania (TFWG) mara baada ya kufungua mkuatano huo uliohusisha
wadau mbalimbali wa misitu kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali
pamoja na Waandishi wa Habarai.
“Kwenye mitandao tunaona video
inasambaa kuonesha bodaboda zimepangana zimebeba magunia mengi ya mkaa ambayo
yana ujazo mkubwa sana hata sisi wenyewe tumeshakutana na watu wanaouza mkaa
kwa Pikipiki huko mitaani yale magunia ni zaidi ya Kilo 50 ambazo zinatamkwa na
sheria kuuzwa kwa shilingi 12,500/- huko yanakozalishwa na mkaa huo unatoka
kwenye maeneo ambayo yanzalisha mkaa kiholela ambako hawazingatii vipimo na
kwepa kununua kwenye maeneo rasmi ya kuzalisha mkaa kiuendelevu hii ni hatari
kwa usalama wa mistu yetu” alifafanua bwana Lyimo.
Amesema kuwa kwenye maeneo ya vijini
ambayo vinatekeleza mradi wa Usimamizi shirikishi wa misitu na Mkaa endelevu
gunia la kilo 50 linauzwa shilingi elfu 12,500/- kama GN417 inavyoonesha lakini
wafanyabishara hawaendi kwenye maeneo hayo wanakimbilia maeneo yanayofanya
biashara ya mkaa usio rasmi na kupata magunia hayo makubwa yasiyofuata vipimo na
hivyo kuzidi kuchochea uharibifu wa misitu ya vijiji huku kule kunakozalishwa
mkaa rasmi kwa kufuata taratibu kukikosa wateja na kukata tamaa.
Amesema kuwa endapo Mkaa utauzwa kwa kilo na
kuwa kwenye mifuko maalumu kutasaidia kupungua kwa uharibifu wa misitu kwenye
maeneo mengi nchini lakini pia kuwepo na utaratibu wa kuwatambua wafanya biashara
hiyo na kujua mkaa unaouzwa umetoka wapi na Kijiji gani ili kuweza kudhibiti
biashara holela ya mkaa nchini ambayo ni hatari kwa afya ya misitu na
mazingira.
Kwa upande wake Afisa Sera na
majadiliano wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) Bi.
Elida Fundi amesema uharibifu wa mistu unaendelea kuongezeka kila kona na hivyo
kuomba wadau kushirikiana kuokoa misitu na kuisaidia nchi.
Afisa Sera na majadiliano wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) Bi. Elida Fundi akiongea na Waandishi wa Habari nje ya mkutano huo (hawapo pichani). |
“Ukiangalia kwa uzoefu wetu tumeona
kwenye maeneo ambayo tunatekeleza mradi wa Usimamizi shirikishi wa misitu na
Mkaa endelevu kumekuwa na mafanikio makubwa sana kwenye kuhifadhi misitu ya
vijiji kupitia wananchi wenyewe kwakuwa wanapata motisha na kuona thamani ya
misitu moja kwa moja kwa kupata ajira na kuteleza miradi mbalimbali ya
maendeleo kijijini lakini mradi ukiondoka mambo yanaharibika” alieleza
Bi.Elida.
Amesema changamoto kubwa ni matumizi
mabaya ya fedha zinazopatikana kutokana na biashara ya Mkaa na Mbao zilizovunwa
kiuendeelevu kwa kufuta misingi i liyowekwa na mradi maana vijiji vimeweza kupata
mapato hadi kufikia shilingi milioni100 na hivyo viongozi kuanza kutolea macho
fedha hizo na kutoka nje ya utaratibu.
Afisa Majadiliano na Sera huyo wa
MJUMITA amesema bado nguvu ya pamoja inahitajika katika usimamizi wa misitu na
fedha zinazopatikana kutokana na uvunaji wa mkaa na mbao lakini pia kuzuia
maeneo mengine ambayo hayana mfumo rasmi wa uvunaji kuacha uvunaji huo holela
ambao unavutia wateja kwenda huko na kukimbia maeneo ya vijiji ambavyo
vinafuata taratibu na mfumo mzuri ambao umewekwa unaochangia kwenya mapato ya
jamii,vijiji, Halmashauri na Serikali kuu kupitia tozo na kodi.
TFCG na MJUMITA wanatekeeleza Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamiii(USMJ) chini ya Mradi wa kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) na mradi wa kuhifadhi Misitu kwa kuwezesha biashara endelevu ya Misitu (CoFOREAT) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC).
Aina za Magunia ya Mkaa yanayozalishwa kwenye maeneo yasiyo rasmi yanavyojazwa bila kuzingatia uzito na kuuzwa kwenye maeneo mbalimbali mijini. |
0 Comments