Na: Ayoub Mwigune
imeelezwa kuwa kushiriki katika mazoezi mbalimbali ya mwili huchangia kufanya mwili kuwa na afya na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi kwani mazoezi husaidia kupambana na magonjwa yasiyoambukiza vilevile kuondoa mawazo yanaweza kupelekea kushiriki katika makundi na vitendo visivyofaa katika jamii.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba wakati wa kuhitimisha Bonanza la michezo maarufu kama VC CUP katika viunga vya Kampasi ya Edward Moringe Morogoro ikiwa ni utaratibu wa SUA kuhakikisha wafanyakazi wa chuo hicho wanashiriki katika michezo ili kuupa mwili afya na ufanisi katika kazi kila mwaka.
Awali Prof. Komba amepongeza Menejimenti ya Chuo hicho kwa kuthamini michezo na kuanzisha mashindano hayo yenye lengo kuwaunganisha wafanyakazi wote wa SUA kupitia michezo ili kufahamiana na kuondoa mawazo mabaya pamoja na kujenga afya zao.
‘’ Natambua kuwa lengo kuu la Taasisi ya Elimu kama hii ni Taaluma lakini naomba Niipongeze sana menejimenti na uongozi wa SUA kwa kulipatia kipaumbele swala la michezo kwa wafanyakazi Chuoni hii ni hatua nzuri kwani itaongeza ufanisi na ari ya wanajumuiya wa SUA kushiriki kwenye michezo” Alissema Prof. Komba .
Aidha Prof. Komba amewasihi wafanyakazi wa Chuo hicho kuweza kuitumia vizuri michezo katika kuimarisha uhusiano na kubadilishana uzoefu katika kazi kwani kupitia michezo ni rahisi kurahisha mawasiliano huku akiongeza kusema kuwa kwa sasa michezo imekuwa ni sehemu ya ajira kwa kuweza kuajiri vijana mbalimbali huku akitolea mfano wa waamuzi waliochezesha michezo hiyo.
Vilevile Prof. Komba ametoa Tsh 500,000 kwa ajili ya kusaidia timu ya wafanyakazi wa SUA inayokwenda kushiriki katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Kampuni binafsi Tanzania (SHIMUTA) ambayo yameanza kufanyika Jijini Tanga leo tarehe 16 Novemba 2022 .
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga michezo hiyo Rasi wa ndaki ya Solomon Mahlangu Prof. Geoffrey. Karugila kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphaelamesema lengo la michezo hiyo ni sehemu ya Chuo kupata wanamichezo ambao watakiwakilisha Chuo kwenye michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi lakini pia kuimarisha uhusiano wa wafanyakazi katika idara mbaimbali sambamba pamoja kujenga afya zao .
Pamoja na hayo Prof. Karugila kupitia mashindano hayo wameendelea kuboresha uhusiano na Taasisi mbalimbalimbali huku akitolea mfano wa Benki ya CRDB na Chuo hicho ambapo benki hiyo wameendelea kuwa wadhamini wa mashindano hayo kwa muda mrefu.
0 Comments