Na: Calvin Gwabara - Morogoro.
Wanachama wa
Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu Tanzania MJUMITA wametakiwa
kushirikiana na Serikali kwenye kampeni ya kuitunza misitu ya asili na kurejesha
uoto wa asili ili kuifanya Tanzania ya kijani ifikapo mwaka 2030.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja wakati akifungua Warsha na Mkutano Mkuu wa 22 wa mwaka wa MJUMITA Mkoani Morogoro. |
Kauli hiyo imetolewe
na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja wakati akifungua
Warsha na Mkutano Mkuu wa 22 wa mwaka wa MJUMITA unaofanyika Mkoani Morogoro
kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji na kupanga mikakati mipya ya
usimamizi wa misitu nchini.
“Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani anapambana
kuhakikisha swala la uhifadhi wa misitu na mazingira nchini linasimamiwa vizuri
ndio maana kila mara amekuwa akizungumzia swala hili kila anapokwenda
kuzungumza na Wananchi hivyo kwakuwa na nyinyi hapa mnatoka kanda zote nchi nchi
nzima lazima tuanzishe kampeni maalualumu kuunga mkono jitihada za Rais wetu
katika kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na hii iwe Kijiji kwa Kijiji,nyumba
kwa nyumba, Kitanda kwa kiatanda na shuka kwa shuka naamini haitashindwa nan
chi itakuwa ya kijani tena” alisema Mhe. Masanja.
Amesema
anatambua kuwa miti inafika wakati inakomaa na inafaa kuvunwa ili jamii
inufaike nayo kwa kupata mazao mbalimbali lakini lazima uvunaji huo uzingatie
utaalamu na uvunaji kwa uendelevu kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho.
Aidha naibu Waziri
huo wa Maliasili na utalii amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA na wataalamu
wake kwa kuanzisha mtandao huu ambao sasa umefikisha miaka 22 anaamini kuwa
hadi itakapofika mwaka 2030 misitu yote ya Tanzania itarudi na hivyo kuwataka
Washiriki wote kuondoka na dhamira kuwa wanakwenda kurudisha uoto wa Asili.
Awali Mwenyekiti wa MJUMITA Bi. Rehema Ngalekele amesema Mtandao huo ulianzishwa
mwaka 2000 na kusajiliwa kama NGO mwaka 2007 na ina wanachama mitandao 120 kwenye
kanda sita Tanzania bara na umeleta pamoja wanachama takribani 15,000 katika
usimamizi wa misitu ya asili ipatayo hekta 1,800,000 katika vijiji zaidi ya 450
na kuboresha Maisha ya jamii kupitia shughuli mbalimbali kama vile ufugaji
nyuki,Kilimo hifadhi,Miradi ya maji,ufugaji wa vipepeo, uanzishwaji wa VICOBA na
kufanikisha mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye vijiji zaidi ya 100 huko
kilosa,Lindi,Liwale,Nachingwea, Handeni na Mvomero.
Mwenyekiti wa MJUMITA Bi. Rehema Ngalekele akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni rasmi. |
“MJUMITA tunapenda
kutoa pongezi kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mma yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake
kubwa na nzuri anazozifanya kwa kupambana
na janga la mabadiliko ya Tabianchi na kuhakikisha rasilimali za nchi
zinalindwa na kusimamiwa kwa Madhubuti kwa maslahi ya kizazi cha sasa na
kijacho”alisema Bi. Ngalekele.
Akieleza
lengo la Mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA Bi. Rahima Njaidi amesema kuwa
ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa misitu wakiwemo Wanachama na Wananchi
kutoka mikoa 13 ya Tanzania Bara kwenye Wilaya 30 na vijiji zaidi ya 450 ambao
wanahifadhi misitu ya vijiji na kuivuna kwa njia endelevu.
Mkurugenzi Mtendaji wa MJUMITA Bi. Rahima Njaidi akieleza malengo ya Warsha na mkutano huo wa mwaka wa 22 wa MJUMITA. |
“Kwa mwaka huu tunajaribu kuongelea zaidi swala la ushirikishi wa Wanawake na Vijana katika uhifadhi wah ii misitu lakini pia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na makundi haya mawili mara nyingi yansahaulika ingawa yanamchango mkubwa sana katika kuendeleza sekta ya misitu” Alisema Bi. Njaidi.
Aidha amesema wapo hapo kwaajili ya kuweka mikakati Madhubuti ya kuhakikisha makundi hayo yanasihrikishwa kikamilifu katika kutunza misitu lakini pia na wao wenyewe wananufaika na ndio maana wapo na wadau mbalimbali kamavile TFCG,WWF,Plan CANTZ,FORVAC na MCDI na wengine ili kila mmoja akirudi mahali pake pa kazi akatekeelze maazimio hayo.
Mlezi wa MJUMITA Bwana Charles Meshack akitoa neno la shukrani kwa Mgeni rasmi. |
MATUKIO KATIKA PICHA YA WAJUMBE WAKIFUATILIA HOTUBA ZA UFUNGUZI WA MKUTANO HUO.
0 Comments