Na: Calvin Gwabara.
Serikali
ya Tanzania inapoteza kiasi cha shilingi bilioni 463 kwa mwaka kutokana na
mapato yatokanayo na kodi na tozo mbalimbali za mauzo ya biashara ya Mkaa
nchini kwenye tani 1,895,248 sawa na kilo bilioni 1.89 zilizoripotiwa
kuzalishwa mwaka 2021.
Hayo yamefafanuliwa na Afisa Kujenga uwezo kutoka Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Bwana Simon Lugazo wakati akiwasilisha mada kuhusu ushahidi wa matokeo hasi ya kubadilika kwa kanuni ikiwemo GN417 usimamizi wa misitu ya jamii na mchango wake kwenye uchumi wa taifa wakati wa mkutano wa Wadau na Wanachama wa Kikosi Kazi cha Misitu Tanzania (TFWG) uliofanyika Mkoani Morogoro.
“Kwa
mujibu wa ripoti ya Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka
2021 imebainisha kuwa thamani ya biashara ya Mkaa nchini ni shilingi 2,056,771,556,434
ambapo katika fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 9.9 ni tozo na kodi
iliyokusanya na kuingia serikalini kutokana na mkaa unazalishwa nje ya vijiji
vyenye usimamizi shirikishiwa misitu ya jamii hizi ni zile zilizokamatwa na
kupita kihalali lakini mkaa mwingi zaidi ya huo unapita kwa njia za magendo na
unavunwa kwa njia zisizo halali ambao tunauona unapita na mapikipiki kuelekea
mijini” alifafanua Simon.
Afisa
huyo mjenga uwezo wa TFCG amesema awali kulikuwa na mafanikio makubwa katika
uhifadhi Misitu ya Vijiji kupitia mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu
Jamii kupitia uvunaji endelevu wa biashara ya Mkaaa na mbao na kuchangia jamii
kuhifadhi na kulinda misitu na kupata fedha za kutelekeza miradi mbalimbali ya
maendeleo kwenye vijiji kutokana na
mapato hayo lakini baada ya ujio wa GN417 uzalishaji na usimamizi umeshuka
kwakuwa jamii haipati tena motisha.
Amefafanua
kuwa awali kabla ya ujio wa GN417 Serikali za vijiji yalijengewa uwezo na kupewa mamlaka ya
kuanzisha na kufanya shuhuli za uvunaji kwenye misitu ya vijiji kwa njia
endelevu na kupanga bei za kuuza mazao hayo ya misitu hususani mkaa na mbao
kupitia sharia ya misitu ibara ya 49(6) kwa kutoa vibali vya uvunaji na kupanga
bei.
“Mkaa
endelevu kwenye vijiji 30 vya Mkoa wa Morogoro ambavyo vinatekeleza mradi wa
mkaa endelevu na usimamizi shirikishi wa misitu ya vijiji kati ya mwezi wa 12
mwaka 2015 hadi septemba mwaka 2021 yameonesha kuwa yameanguka kwa baada ya
ujio wa GN417 katikati mwa mwaka 2019 kwa shilingi bilioni 1.3 kwa kwa kipindi
cha miezi 24.
Amefafanua
kuwa hali hiyo inatokana na kwamba gunia moja la Mkaa kwa bei ya Serikali linatakiwa kuuzwa kwa shilingi 42,648 ambayo
ndio bei inayojumlisha kodi na tozo mbalimbali zilizo rasmi zaa serikali wakati
mkaa unauzwa kwa shilingi elfu 30,420 kwenye maeneo ambayo hayana mfumo huo wa
uhifadhi shirikishi wa misitu na uvunaji endelevu wa mkaa hali ambayo
inawafanya wanunuzi kukimbilia kwenye maeneo hayo yanayovuna bila kuzingatia
uendelevu wa misitu wala usimamizi.
Mtaalamu
huyo amesema kwa mujibu wa utafiti walioufanya ulionesha kuwa mwaka 2018 kulikuwa
na miradi 43 yenye thama ni za zaidi ya shilingi milioni 229 iliyokuwa
inatekelezwa kutokana na biashara ya Mkaa kwenye vijiji 30 vya mradi Mkoani
Morogoro lakini baada ya ujio wa GN417 miradi imeshuka hadi kufikia million 13
pekee.
Kwa
upande wake Afisa Maliasili wa Mkoa wa Morogoro Bwana Joseph Chuwa amesema
GN417 ni ya Tanzania nzima sio vijiji vinavyotekeleza mradi pakee na ili
kukomesha tatizo hilo ni muhimu sasa kuongeza nguvu katika kudhibiti maeneo
ambayo yanachoma mkaa kwa njia holela ili mkaa uweze kutoka kwenye vijiji
vyenye mpango wa usimamaizi shirikishi wa misitu na uvunaji endelevu.
Amesema Sera na Sharia za Misitu ni za Tanzania nzima hivyo ni vyema kukawa na mfumo mmoja wa usimamizi wa Misitu yote Tanzania kutoka Misitu ya Serikali mpaka ya mtu binafsi hii haina maana kuwa inaondoa haki ya umiliki wa mtu mmojammoja bali isaidie kudhibiti na kusimamia Misitu yote.
“Asilimia
48 hadi 50 ya Misitu yote ambayo ipo hatarini kutoweka ipo kwenye ardhi za
vijiji na inapungua kila mwaka nadhani kuwe na ubia kwa maana ya Serikali
kuu,TFS,Halmashauri na Vijiji vyenyewe kwenye kuisiamamia hii Misitu ya vijiji
maana kwa mtazamo wangu naona kama uwezo wa vijiji kuisimamia unakuwa mdogo kwa
maana ya vitendea kazi,fedha na utaalamu”alisema Chuwa.
Aliongeza
“Hii izingatie pia kwenye kugawana keki itokanayo na Misitu hiyo kwa maana
vijiji vyenyewe vipate mgao mkubwa, Halmashauri nazo zipate mgao na hivyohivyo
kwa TFS na Serikali kuu kwahiyo kila mmoja ataona Misitu ina faida kwake na
kuongeza nguvu kwenye uhifadhi wa misitu hiyo isivunwe kiholela kama ilivyo
sasa”.
0 Comments