SUAMEDIA

Bodi ya wahandisi (ERB) kujenga Kituo cha Umahili cha Wakandarasi

 

Na Stanslaus Likomawagi

Dodoma

Bodi ya wahandisi (ERB) inatarajia kujenga Kituo cha Umahili cha Wakandarasi katika eneo la Kizota Jijini Dodoma ili kuendelea kukuza na kuendelea na kuifanya taaluma hiyo kwenda sambamba na mabadiliko yanayotokea.


Msajili wa Bodi (ERB) Mhandisi Benard Kavishe katika moja ya mikutano yake (Picha - Michuzi Blog)

Msajili wa Bodi hiyo Mhandisi Benard Kavishe ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma November 10 2022 alipokuwa akiwaeleza waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo.

Amesema kuwa kituo hicho cha umahili chenye lengo la kuendelea kuwapika  wakandarasi kitakuwa na maabara, karakana za umeme na mambo mengine lakini pia kutakuwa na hosteli

Mhandisi Kavishe  ametaja vipaumbele vya bodi hiyo kwa mwaka huu kuwa ni kuhuisha leseni kwa wakandarasi,kudhibiti wakandarasi wa ndani na nje ya nchi ili kuleta tija katika kutekelea miradi mbalimbali

Mhandisi Kavishe ametoa wito kwa wahandisi wote kuwa waadili na kuepukana na vitendo vinayokwenda kinyume na kiapo cha taaluma yao kwa maslahi mapana ya taifa.

Post a Comment

0 Comments