Na: Tatyana Celestine
Wafugaji
nchini wametakiwa kuanza kutumia Teknolojia ya Unyonyeshaji wa Ndama
wa Ng`ombe, Mbuzi na Kondoo ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuongeza tija
katika Sekta ya ufugaji pasi kuendelea kutumia mazoea yanayopelekea vifo kwa wanyama hao wadogo pindi wanapokubwa na changamoto ya lishe hasa kwa upande wa
Maziwa.
Hayo
yamesemwa na Mhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), ambaye kwa
sasa ni Daktari wa Mifugo kutoka Kampuni ya Farmbase Limited Dkt. Abdul Khamis
Byarugaba wakati wa ziara yake katika mashamba ya wafugaji Wilaya
ya Kisarawe jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuwapa elimu ya matumizi
sahihi ya dawa na lishe katika ufugaji.
Dr.
Byarugaba ametaja malengo mengine kuwa ni kusaidia kutatua
changamoto zinazowakumba na kuwashauri njia sahihi ya kuwatunza Ndama ili wawe na afya hata ikiwa wazazi wao wamekumbwa na changamoto ya
maradhi au kupoteza uhai.
Dr.
Byarugaba ametaadhalisha kuwa ndama wengi wanapoteza maisha kipindi ambapo
wafugaji wanakosa nyenzo sahihi za kuwasaidia kuweza kupata maziwa kama
inavyotakiwa hivyo amewataka kutumia teknolojia hiyo ya kunyonyeshea wanyama
iliyotengenezwa maalumu ili kuweza kunyonyesha mnyama zaidi ya mmoja kwa mara
moja.
Aidha
ametaja faida ya kutumia teknolojia hiyo kuwa ni kuongeza thamani ya mifugo kwa
mfugaji kuwa na uwezo wa kukadiria kiasi sahihi cha maziwa ya
kulisha ndama wa ng`ombe, mbuzi au kondoo wadogo, kuepusha maambukizi ya
maradhi kutoka kwa mama kwenda kwa ndama na hivyo kupelekea kumuongezea thamani
ya mifugo na kuuza Wanyama wenye afya kwa gharama aipendayo.
Dr.Byarugaba
amewashauri wafugaji kuhakikisha wanatumia dhana za mifugo zenye ubora
zinazopatikana kwa uhakika na urahisi nchini kupitia kampuni ya Farmbase pekee
ambao wanazalisha, wanagiza na kusambaza bidhaa ili kurahisisha kuepuka
changamoto za kupoteza fedha pasipo faida.
0 Comments