Na:Winfrida Nicolaus
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) katika kuelekea maazimisho ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kimeendelea kutendea kazi yale yaliyokuwa maono yake ya kuhakikisha kinatatua changamoto mbalimbali ambazo wakulima wanakumbana nazo vilevile kuchangia katika kuimarisha uzalishaji kwa maendeleo ya mtu mmojammoja na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisini kwake kuhusu maono ya Mwalimu Julius Nyerere katika kuhakikisha Sekta ya Kilimo inakua vilevile kunakuwa na wataalam wa kilimo wa kutosha ili waweze kutatua changamoto za wakulima na kunakuwa uzalishaji wa kutosha.
Amesema maono ya Mwalimu yalikuwa ni kuanzisha chuo ambacho sio tu kingezalisha wataalam katika maeneo mbalimbali yanayohusiana na kilimo vilevile kingefanya tafiti za kuweza kutatua changamoto ambazo wakulima wanakumbana nazo hivyo SUA hii leo kwa kupitia Baraza la linalo simamiwa na Mwenyekiti wa Baraza Mhe. Jaji Mstaafu Othaman Chande
Prof. Chibunda amesema mbali na kufundisha kuna uhakika kwamba asilimia 99 ya Maafisa Kilimo na wataalam wa Kilimo, Misitu, Mifugo, Uvuvi na Mazingira katika nchi ya Tanzania wengi wao ni wahitimu wa SUA na kuongeza kuwa SUA imeendelea kulitendea kazi jukumu waliyopewa na maono na matamanio ya Mwalimu Julius Nyerere.
‘‘Mwalimu Nyerere alitamani kuona watanzania wanakuwa na uwezo wa kujitegemea hasa kwenye upatikanaji wa chakula ambapo aliweza kuja na rogramu tofauti kwaajili ya kuendeleza Kilimo nchini hivyo taasisi mbalimbali za mafunzo ya uelimishaji ili wananchi waweze kupata Elimu inayofaa ya Kilimo ambacho kitakuwa na Tija zilianzishwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kikiwemo’’, amesema Prof. Raphael Chibunda
‘‘Novemba 4, 1984 baada ya ma majadiliano marefu Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha sheria ya kuunda Chuo Kikuu cha SUA ambacho kilianzishwa kwa dhumuni la ukuzaji na usambazaji wa ujuzi na utaalam wa vitendo katika kiwango cha juu kwa kwenda kuwasaidia moja kwa moja wakulima wakulima wetu na taifa la sasa na badae’’, amesisitiza Prof. Raphael Chibunda
Ameongeza kuwa Sekta ya Kilimo nchini imekuwa na unaweza kukiona kilimo katika nyanja zaidi ya moja hasa kwenye upatikanaji wa mazao na bei ambapo kipindi cha nyuma ulikuwa ni mdogo na kusababisha hata baadhi ya familia kushindwa kumudu mfano mchele lakini kwa sasa uzalishaji umeongezeka na imefika mahali bei ya mchele na unga wa sembe karibu vinaendana bei.
Hata hivyo amesema upatikanaji rahisi wa bidhaa za chakula ambao umetokana na uzalishaji mwingi ni kutokana na juhudi kubwa iliyofanywa na Serikari lakini vilevile kupitia watafiti ambapo kumesababisha mkulima kulima kilimo cha muda mfupi pamoja na kupata au kuvuna zaidi katika eneo dogo ukilinganisha na hapo awali.
0 Comments