SUAMEDIA

Watumishi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania wafanya ziara SUA ili kujifunza na kuona programu zinazofanyika

 

Na: Winfrida Nicolaus

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kinajivunia Utajiri wao unaotokana na uzalishaji wanaoufanya kutoka kwenye Elimu kwa njia ya Vitendo inayotolewa chuoni hapo pamoja na matokeo ya Tafiti wanazozifanya ambapo licha ya kunufaisha jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla vilevile inanufaisha na Jumuiya ya Chuo.

Amebainisha hayo Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda wakati akizungumza na Watumishi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Kampasi Kuu ya Edward Moringe Sokoine, walipofanya ziara chuoni hapo kwa lengo la kujifunza na kuona programu ambazo zinafanyika chuoni hapo.

Amesema licha ya mazao yatokanayo na mifugo pamoja na Kilimo yaliyopo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi, ufanyaji wa Tafiti na Mapato ya chuo vilevile mazao hayo pia hutumika kwaajili ya kuwanufaisha wafanyakazi pamoja na wanafunzi chuoni hapo.

Prof. Chibunda amesema kwa upande wa Mafunzo kwa Vitendo, wanafunzi wao wa mwaka wa pili wanabaki kwa ajili ya mafunzo kwenye mashamba ya chuo na pindi wanapomaliza mafunzo na kufanya kazi nzuri wanapatiwa ng'ombe wawili kwa ajili ya kuwapongeza na kuwafanya wajisikie vizuri kusoma SUA.

‘‘Sisi huwa tunajihesabu kuwa ni Chuo Tajiri, mfano tuna mashindano yetu ya ndani sisi kwa sisi yaani College kwa College na sasa hivi yanaendelea ambayo tunayaita 'Vice Chancellor Cup' ambapo tukifika mwisho timu zilizoshinda tunachinja ngombe wakubwa wawili na kila mwaka lazima tuwaandae kwenye mashamba yetu mawili ya ng'ombe kwaajili ya kuliwa’’, amesema Prof. Raphael Chibunda

Ameongeza katika kutekeleza majukumu yao kutokana na mafunzo yanayotolewa chuoni hapo pamoja na Tafiti kushirikiana na Taasisi pamoja na Mashirika mbalimbali kama TALIRI, TARI, TOSCI, KAMATEK na wengine ambao hufanya nao kazi kwa karibu ili kuhakikisha wanafanya kazi zenye ubora.

Vilevile Prof. Chibunda amesema licha ya mashirikiano mazuri na Taasisi na mashirika mbalimbali kuna vitu vingi ambavyo wanavifanya kama chuo vingine vikiwa ni matokeo ya Tafiti zao ambapo baadhi huvifanya kama biashara mfano katika shamba lao mikonge lenye takribani hekta 200 wanauza Nyuzi, Ng'ombe Mitamba pamoja na Samaki.

‘‘Suwala lingine linaloendana na hilo kuna vituo ambavyo vipo sehemu mbalimbali ya nchi yetu na vituo hivyo vipo kutokana na maamuzi ya makusudi kabisa ya chuo ili kuinufaisha jamii, kwa mfano mnapoenda sehemu yoyote kwa ajili ya kusaidia labda mifugo hauwezi kuwaambia mfano watu wa Njombe waje Morogoro kwaajili ya kujifunza, ndio maana vituo hivyo vipo kwaajili ya kutusaidia kutoa mafunzo karibu kabisa na jamii husika" ameongeza Prof. Raphael Chibunda.

Katika Ziara hiyo ya Watumishi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) wametembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Kitengo cha Samaki, Hospitali ya Rufaa

Taifa ya Wanyama pamoja na Kitengo Atamizi na kupongeza kazi kubwa

ambayo imefanya na SUA .

PICHA NA TATYANA CELESTINE





























Post a Comment

0 Comments