SUAMEDIA

Mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Wanasayansi wa Mazao na Vipando Tanzania kutasaidia kuunganisha Wadau wa Kilimo

NA;  Ayoub Mwigune 

Imeelezwa kuwa Mkutano wa Mwaka wa Umoja wa Wanasayansi wa Mazao na Vipando Tanzania (CROSAT] utasaidia kwa kiasi kikubwa kuunganisha Wataalam wa Kilimo, Wakulima naMakampuni yanayo husika na uchakataji wa mazao ya Kilimo na kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Mazao.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa CROSAT Prof. Kalunde Sibuga ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wakati akizungumza na SUAMEDIA jijini Dodoma kuhusu umuhimu wa Mkutano huo katika Ustawi wa Kilimo nchini.

Awali akielezea kuhusu dhumuni la Mkutano huo Prof. Sibuga amesema ni kupanga mikakati pamoja kuhusu kuboresha Katiba yao ili kuongeza tija katika kilimo cha mazao, kubadilishana mawazo na kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Mazao.

Aidha Prof. Sibuga amesema CROSAT inaunganisha Wataalam wa Kilimo, Wakulima, Makampuni yanayo husika na Uchakataji wa mazao ya Kilimo pamoja na Taasisi zinazo husika na masuala mbalimbali yanayohusu kilimo.

Kwa upande wao baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo Patroba Bwire Masatu ambaye ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) SUA na Jenipher Tairo anayesoma Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Kilimo na Mimea wamesema CROSAT ni Jukwaa ambalo linawaunganisha Wanasayansi wa Mazao na Vipando Tanzania na wadau wote kuweza kuwa na Lugha moja katika ustawi wa Kilimo.

Aidha Washiriki hao pia wameomba wale ambao bado hawajajiunga na  CROSAT waweze kujiunga na umoja huo ili kupata jukwaa imara kwa maslahi mapana ya Taifa na Jumuiya ya Kimataifa kwa ujumla maana Kilimo ndio Sekta pekee inayo ajiri watu wengi nchini.



KATIKA VIDEO


Post a Comment

0 Comments