Na: Calvin Gwabara
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema pamoja na Tanzania kutotumia mazao yatokanayo na mbegu za GMO lakini haiwezi kuzuia watafiti wake kufanya tafiti za Mbegu hizo ili kujijengea uwezo kama nchi wa kuweza kuzifahamu
Kauli hiyo ameitoa Jijini Dodoma
wakati akizindua Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
Tanzania TARI yenye wajumbe 10 aliowateua tarehe 24 Agost, 2022 ikiongozwa na
Mwenyekiti wake Dkt. Tausi Mbaga.
“Nchi yetu haitaki GMO lakini
haituzuii kujifunza kuhusu GMO si ndio jamani?Haturuhusu matumizi ya GMO
seeds,lakini hatuzuiliwi kujifunza, nyie watafiti si ndio kazi yenu? Si ndio
jamani, mnaita Bioteknology, sasa tuna kituo gani cha kwetu ambacho kime
specialize kwenye hii teknolojia ili tuhifadhi tujue, kwenye Pamba kuna hii
inaitwa Bt. Technology, kwa hiyo tujiandae maana Kenya wanai approve na Uganda watai approve sawa eeh, swali letu
la kujiuliza ni namna gani tunaizuia isiingie Tanzania”, alisema Mhe. Bashe.
Mhe. Bashe amesema takwimu
zinasema mwaka 2030 Afrika itakuwa na watu bilioni 1.8 na mwaka 2050 wanaweza
kufika watu Bilioni 2 na hivyo uhitaji wa chakula duniani utaongezeka kwa zaidi
ya asilimia 50 lakini uzalishaji utashuka kutokana na masuala ya kimazingira
kwa hiyo ni lazima kijiandaa wenyewe.
“Mhe. Rais ametupa malengo ya kufikia kukua
kwa kiwango cha asilimia 10 na hatuwezi kuifikia kama hatutafungua tatizo la
mbegu kwenye nchi yetu, tunazo mbegu zetu za asili na ninaomba hili watafiti
mnisikilize kwanza ninapohubiri mbegu ya asili sisemi kwamba tusizalishe mbegu
za kisasa ninachosema ni hivi ni lazima tufike mahali tuifanye sekta yetu ya
mbegu impe chaguo mkulima kwa kile anachotaka kukitumia”, alisisitiza Waziri wa
Kilimo.
Mhe. Bashe amesema kuwa TARI na
watafiti wengine ndio nguzo ya Utafiti na Maendeleo hivyo amewataka kufikiria
zaidi maana anataka Tanzania kuwa wauzaji na wasafirishaji wa mbegu baada ya
kupata Cheti cha uthibitisho wa kuruhusiwa kuuza mbegu nje ya mipaka ya
Tanzania.
KATIKA VIDEO
0 Comments